Na Neema Kandoro Mwanza.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi na Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndg. Velji AminMohamed maarufu kama Mlete Mzungu ametoa madaftari kwa wanafunzi waliokuwa hawana Madaftari ili kuwawezesha kuanza masomo
Mjumbe huyo amewataka Watanzania wengine kusaidia mahitaji ya shule kwa wanafunzi ambao bado wanauhitaji wa vitendea kazi vya shuleni Ili waweze kutimiza ndoto zao.
Alisema kuwa lengo lake ni kuhakikisha kuwa anawasaidia watoto wote wenye mahitaji ili waweze kuanza masomo katika muda muafaka ili wasiweze kuachwa na ratiba ya mitaala ya masomo
Velji Amin Mohamed amekuwa akijitoa kusaidia watu wenye uhitaji ikiwa pamoja na wanafunzi ili waweze kifikia malengo yao ya kimaisha.
Mmoja wa wanafunzi waliopata madaftari alimpongeza kiongozi huyo kwa kuwajali katika kipindi ambacho wanatakiwa kwenda shuleni
“Nilikuwa nimeisha kata tamaaa ya kuendelea na masomo kutokana na Wazazi wangu kutokuwa na hela ya kuninunulia madaftari lakini kupitia kiongozi huyu nimepata Madaftari” Nelisy Nestory
Wakati huo huo Wanafunzi hao walimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Elimu Bure kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu.