Home Kitaifa RC MTANDA AIPONGEZA WILAYA YA MUSOMA UANDIKISHAJI WANAFUNZI MWAKA 2024

RC MTANDA AIPONGEZA WILAYA YA MUSOMA UANDIKISHAJI WANAFUNZI MWAKA 2024

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Said Mtanda ameipongeza Wilaya ya Musoma kwa kufanya vizuri uandikishaji wa wanafunzi kwa mwaka 2024.

Pongezi hizo amezitoa wakati amezungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya uandikishaji na mapokezi ya wanafunzi wa darasa la awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza hadi kufikia tarehe 17 Januari, 2024.

Mtanda ameeleza kuwa taarifa zinaonyesha kuwa Wilaya ya Musoma kupitia halmashauri zake za Musoma na manispaa ya Musoma zimefanya vizuri katika uandikishaji na mapokezi ya wanafunzi.

Ninaipongeza halmashauri ya Wilaya ya Musoma kwa kuongoza kimkoa katika kuandikisha wanafunzi wa farasa la awali na kidato cha kwanza na manispaa ya Musoma kwa kuongoza katika kuandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza.

Hii ni hatua nzuri ambayo inastahili kupongezwa ili watoto wetu waendelee kupata elimu itakayoweza kuwanufaisha hapo baadae”,amesema Mtanda.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka viongozi wa Wilaya, Halmashauri, Watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha wanafunzi wote waliotarajiwa kuanza masomo kwa mwaka 2024 wanapelekwa shule na wanaanza masomo.

Nitoe wito kwa Wakuu wa Wilaya na viongozi wa ngazi zote kuhakikisha wanafanya msako wa wanafunzi wote wanaotakiwa kwenda shule wanaanza masomo kabla ya mwisho wa muda wa kupokea wanafunzi kwa mwaka 2024”,ameongeza

Mtanda amewapongeza viongozi wote, wasimamizi wa elimu, walimu wakuu na wakuu wa shule kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuwataka kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaotakiwa kuanza masomo wanaanza masomo bila vipingamizi.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Tawala Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bulenga Makwasa imeeleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imeandikisha jumla ya wanafunzi 9,212 ambapo kati yao wavulana ni 4692 na wasichana ni 4520 sawa na asilimia 96.56 ya watoto 9,540 waliotarajiwa kuandikishwa dsrasa la Awali.

Halmashauri nyingine zilizofanya vizuri uandikishaji wa darasa la awali ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti iliyoandikisha kwa asilimia 95.81 na Halmashauri ya Wilaya ya Butiama iliyoandikisha kwa asilimia 91.99.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma pia imefanya vizuri katika uandikishaji wa wanafunzi wa Kidato cha kwanza ambapo imeandikisha wanafunzi 4,092 kati ya wanafunzi 5733 waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na shule za sekondari katika halmashauri hiyo ambayo ni sawa na asilimia 71.

Halmashauri nyingine zilizofanya vuzuri uandikishaji wa kidato cha kwanza ni manispaa ya Musoma asilimia 69.36, halmashauri ya mji wa Bunda asilimia 62.13.

Aidha taarifa hiyo imeonyesha kuwa Manispaa ya Musoma imefanikiwa kuandikisha wanafunzi 4,482 darasa la kjwanza kati ya maoteo ya kuandikisha wanafunzi 4,437 kwa mwaka 2024 ambayo ni sawa na asilimia 101.01.

Halmashauri nyingine zilizofanya vizuri katika uandikishaji wa darasa la kwanza ni halmashauri ya Wilaya ya Serengeti asilimia 99.81, halmashauri ya Wilaya ya Rorya asilimia 96.18.

Uandikishaji wa
wanafunzi unaendelea hadi tarehe 31 March, 2024 ambapo utasitishwa hadi mwaka uandikishaji kwa ajili ya mwaka mwingine wa masomo utakapoanza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!