Home Kitaifa DC NAANO, KAMISHNA WA ARDHI MKOA WA MARA WASIKILIZA MIGOGORO YA ARDHI...

DC NAANO, KAMISHNA WA ARDHI MKOA WA MARA WASIKILIZA MIGOGORO YA ARDHI BUNDA

Na Shomari Binda-Bunda

MKUU wa Wilaya ya Bunda Dk. Vicent Naano na Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Mara Joseph Bitanamani wamewasikiliza wananchi na kutoa majibu ya migogoro ya ardhi.

Zoezi hilo limefanyika kwenye eneo la stend ya zamani mjini Bunda ikiwa ni mwendelezo wa kliniki ya migogoro ya ardhi inayoendelea mkoani Mara.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye kliniki hiyo mkuu wa wilaya ya Bunda Vicent Naano amesema kila kero au mgogoro wowote utasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi.

Amesema serikali inayo nia njema na wananchi katika kumaliza masuala ya migogoro ya ardhi na ndio iliyopelekea kuanzisha kliniki hiyo.

Naano amesema migogoro inapelekea kukwamisha shughuli za kiuchumi kutokana na ufatiliaji wake hivyo ni muhimu kuisikiliza na kuomaliza.

Mkuu huyo wa wiilaya amesema asitokee mtu akafanya ujanja ili apate faida kwenye ardhi bali kila mmoja awe mkweli kwenye kile anachokifatilia.

Naano amesema wananchi wanapaswa kuitumia kliniki kumaliza migogoro na sio kuwasubili viongozi wa kitaifa na kuibua migogoro upya.

“Hapa Bunda tumesikiliza migogoro hadi watu wote wameisha kwa kutoa majibu na hatua za kufuata kwa lengo la kufikia mwisho”

“Kliniki imekwenda vizuri lakini bado nafasi ipo kwa kuwa ofisi ya ardhi ya wilaya na ofisi ya kamishina msaidizi wa mkoa zipo zitaendelea kufanya shuughuli za ardhi”, amesema Naano.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Mara Joseph Bitanamani amesema kila mwananchi amesikilizwa na kupatiwa majibu kutokana na migogoro iliyowasilishwa.

Amesema kwa mwananchi mwenye shida yoyote ya ardhi ofisi yake ipo wazi kwaajili ya kusikiliza na kupatiwa ufumbuzi.

Kupitia kliniki hiyo mkuu wa wilaya ya Bunda na maafusa wa ardhi walipata nafasi ya kutembelea maeneo yenye migogoro kwa kuangalia na kutoa majibu

Baadhi ya wananchi wsliosikilizwa kwenye kliniki hiyo ya Bunda wameishukuru serikali kwa kuwafuata na kusikiliza kero zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!