Theophilida Felician Kagera.
Watanzania wakiazimisha kumbukizi ya mapinduzi ya miaka 60 ya Zanzibar imeelezwa kuwa mapinduzi hayo yamejaa matokeo chanya ya mafanikio kwa wananchi
na nchi kwa ujumla.
Ameyasema hayo mzee wa Kagara na kiongozi mstaafu wa nyadhifa mbalimbali ikiwemo ya uwenyekiti wa CCM Kagera na Ubunge wa Jimbo la Ngara Pius Ngeze wakati akizungumza na Blog hii ya Mzawa ofisini kwake mjini Bukoba.
Mzee Ngeze awali ameanza kwakuelezea kwa ufupi historia ya mapinduzi hayo yaliyomuondoa madarakani Sultani na serikali yake mnamo Tarehe 12 January mwaka 1964.
Amefafanua kuwa aliyeshiriki mapinduzi hayo ni hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwa lengo la kuwakomboa wananchi wa Zanzibar waliokuwa wakitawaliwa kimanyanyaso na utawala wa waarabu chini ya Sultan.
Kwa mjibu wa mzee Ngeze baada ya Karume kufanya mapinduzi matukufu kwa nguvu ya umma na kuwakomboa wananchi, ni faida nyingi zimeendelea kujitokeza zaidi ikiwemo ya amani na upendo kwa wa Tanzania.
Licha ya Amani faida nyingine ameitaja kuwa ni pamoja na ya muungano uliodumu kwa muda mrefu wa nchi mbili za Zanzibar na Tangayika ulioundwa chini ya Karume na Nyerere, na mengine mengi.
“Wakati ule wa Zanzibar waliishi chini ya Sultani hivyo waafrika hawakuheshimiwa, walibaguliwa, walionekana ni vibaraka ndani ya nchi yao, waliowengi walinyanyasika mno kwakweli hali ya Zanzibar ilikuwa niyakunyong’onyezwa sana, na katika kumbukizi hii wenzetu wanafahamu maana ya mapinduzi haya kutokana na madhira yaliyowakuta kipindi cha utawala huo” Amesema Mzee Ngeze.
Ametoa wito akiwasihi wananchi na viongozi kuendelea kuyathamini na kuyaenzi mapinduzi hayo enzi na enzi ili nchi iendelee kutawaliwa kwa misingi ya amani na utulivu kama yalivyokuwa maono ya waasisi wa nchi hizo mbili Karume na Mwalimu Nyerere jambo ambalo litaongeza mafanikio ya ujenzi wa Maendeleo kama ilivyo adhima ya Serikali.