Home Kitaifa TUMIENI UMEME WA REA KUJILETEA MAENDELEO – MBUNGE CHEREHANI

TUMIENI UMEME WA REA KUJILETEA MAENDELEO – MBUNGE CHEREHANI

Na Mathias Canal, Ushetu-Kahama

Mbunge wa jimbo la Ushetu, Mhe. Emannuel Cherehani amewataka wananchi kutumia uwepo wa umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kujiletea maendeleo ya kiuchumi.

Mhe. Mbunge Cherehani ameyasema hayo Januari 11 wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha SabaSabini, Kata ya SabaSabini Halmashauri ya Ushetu, mkoani Shinyanga.

Mhe. Cherehani amesema kuwa mpaka wakati anaingia kwenye nafasi ya Ubunge Novemba 2021 Vijiji 21 pekee ndio vilivyokuwa na umeme na mpaka Januari 2024 Vijiji 78 kati ya Vijiji 112 tayari vina umeme.

“Tunamshukuru Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan maana anahangaika usiku na mchana kuhakikisha tunapata fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo huu mradi wa kusambaza umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)”

“Njia pekee itakayompa faraja Mhe. Rais ni kuona wananchi wake mnajikomboa kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kupitia umeme huu. Tusitumie umeme huu kuwasha taa pekee, bali tubuni na kufanya miradi ya biashara itakayoinua hali ya vijiji vyetu pamoja na uchumi wetu kama kufungua saluni pamoja na miradi mingine.” Amesema Mhe. Mbunge Cherehani.

Mhe. Mbunge Cherehani amesema Vijiji ambavyo umeme haujafika atahakikisha mpaka Machi mwaka huu miundombinu itakuwa ishafika kwa ajili ya kuanza kunufuaika na umeme wa REA kama vilivyo vijiji vingine.

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!