Home Kitaifa WATANZANIA ZAIDI YA 100 WANUFAIKA NA MAGIFTI DABO DABO , FANYA HAYA...

WATANZANIA ZAIDI YA 100 WANUFAIKA NA MAGIFTI DABO DABO , FANYA HAYA BADO UNA NAFASI YA KUSHINDA

 Na Mwandishi Wetu.

Januari 11, 2024 Warda Abdallah Shetui Mjasiliamali Mkazi wa Mwananyamala Dar Es Salaam na Charles Aidan Ngosingosi Fundi Selemala Mkazi wa Tabata – Dar Es Salaam ni baadhi ya Wawakilishi wachache kutoka Dar Es Salaam waliojishindia Milioni Moja Moja na kuingia kwenye Orodha ya zaidi ya Washindi 100 wa kampeni ya MAGIFTI DABO DABO inayoendelea hivi sasa.

Meneja Bidhaa – Tigo Bwn. Eginga Mohammed ( katikati ) katika picha ya pamoja na baadhi ya Washindi wa Milioni Moja Moja Kampeni ya Magifti DABO DABO Droo ya saba , ambapo amesema kuwa hadi sasa Tigo washatoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa Taslim , Vifaa vya Hisense na Safari za Zanzibar na Dubai kwa zaidi ya Watanzania 100 tangu Kampeni izinduliwe.

Ikumbukwe Kampeni hii inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo ilizinduliwa Mwishoni mwa Mwezi Novemba Mwaka jana huku  ikimtambulisha Haji Manara kama SEMAJI la Kampeni hii, ambapo mteja wa Tigo anaweza kushinda Fedha Taslimu hadi Milioni 10, Safari ya Kwenda Dubai au Zanzibar, Set ya Vifaa vya Ndani ambavyo ni Sound bar, Friji, TV na Microwave na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) , kingine kinachovutia katika kampeni hii ni kwamba ukishinda kitu kimoja wapo kati ya ivyo unamchagua na yeyote umpendae ili apewe zawadi iyoiyo uliyoshinda hii ndio maana halisi ya MAGIFTI DABO DABO.

Akizungumza baada ya kuwakabidhi washindi mfano wa Hundi  , Mwakilishi kutoka Tigo Bwn Eginga Mohammed  amewasisitiza  Watanzania kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa ili kuibuka washindi maana kampeni bado inaendelea

” Mwezi Disemba Tigo tuliwapeleka washindi 15  DUBAI , na wengine walienda Zanzibar katika kampeni hii hii” wapo pia waliojishindia Pesa Taslimu na wapo pia wamejishindia Vifaa vya Hisense. kwahyo kampeni bado inaendelea fanyeni miamala na TIGO PESA kwa wingi, Lipa kwa Simu, nunua vifurushi ili utengeneze mazingira ya kuibuka Mshindi ” amesema Eginga Mohammed .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!