Theophilida Felician Kagera.
Mkuu wa wilaya Bukoba Mhe Erasto Sima atangaza msako mkali wa kuwabaini watoto wote ambao hawajaripoti shule kuanza masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2024 shule za Sekondari Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.
Ametoa kauli hiyo mbele ya wananchi kata ya Kashai katika mwendelezo wake wa kufanya ziara ya kupokea kero za wananchi kata zote za Manispaa ya Bukoba.
Ameeleza kuwa kutokana na baadhi ya wazazi na walezi kwenda kwa mwendo wa kuchechemea katika kuwapeleka shule watoto wao waliochaguliwa kujiunga na msomo ya sekondari ifikapo Tarehe 22 mwezi wa January mwaka huu wa 2024 Serikali itaanza msako wa nyumba kwa nyumba ili kuwapata watoto wote ambao hawajapelekwa shule.
“Nawambieni hatutahangaika na watoto tutahangaika nayinyi wazazi haiwezikani watoto hawapo shule sisi tukasita kuchukua hatua,
Rais wetu Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani ameleta mabilioni mengi ya fedha hapa kwa ajili ya kuwezesha sekta ya Elimu zaidi madarasa ya mejengwa na kukamilika nyie mnashindwa kuwapeleka watoto wakasome haiwezikani tutawashughulikia tuu” amesema Mkuu wa wilaya Sima.
Ametolea mfano wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari Samia iliyopo kata hiyo ya Kashai kuwa hali inasikitisha sana idadi ya waliochaguliwa ni 98 walioriopoti tangu Tarehe 8 hadi sasa Tarehe 11 ni wavulana 14 na wasichana 10 na shule ya sekondari Kashai idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ni 550 na zimechukuliwa fomu 459 hadi leo hii walio ripoti na kuanza masomo wavulana 148 na wasichana 157 nakupelelekea kufika idadi ya wanafunzi 305 sawa na asilimia 54.4%
“Idadi ya wanafunzi hawa siyo nzuri niendelee kusisitiza tutasawaka popote pale walipo mnaniona naongea kwa upole mtayaona matokeo ya upole huu juu ya hili wazazi na walezi wapelekeni watoto shule ili wakapate haki yao ya elimu Serikali imeishawajengea madarasa ya kutosha nakuweka miuondo mbinu ya madawati yakutosha pia” ameendelea kwa msistizo kiongozi huyo.
Hata hivyo amewasihi wananchi kwa pamoja kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais katika mambo mbalimbali ya ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa Bukoba na kwingineko.