Home Kitaifa AHADI YA MBUNGE MATHAYO UCHIMBAJI WA MITARO ENEO LA KARIAKOO YAANZA KUTEKELEZWA

AHADI YA MBUNGE MATHAYO UCHIMBAJI WA MITARO ENEO LA KARIAKOO YAANZA KUTEKELEZWA

Na Shomari Binda-Musoma

AHADI iliyotolewa wiki iliyopita na mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ya uchimbaji wa mitaro kwaajili ya kupitisha maji imeanza kutekelezwa.

Mitaro hiyo imeanza kuchimbwa kwenye eneo la Kariakoo manispaa ya Musoma ambapo maji ya mvua yamekuwa na adha kubwa kwa wananchi wanaoishi na wafanyabiashara wa eneo hilo.

Kamera ya Mzawa Blog imeshuhudia “greda” likiendelea na kazi ya kuchimba mtaro kuanzia eneo la Kariakoo senta kuelekea mtaa wa machinjioni.

Wiki iliyopita mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo alifanya ziara ya kutembelea Kata ya Bweri na Rwamlimi kwenye miundombinu iliyohalibiwa na mvua na kuahidi kufanyiwa ufumbuzi mara moja.

Alisema athari za mvua ameziona kwenye maeneo ya Kariakoo na Machinjioni na kwa muda mfupi bila kusubili bajeti ya Tarura atayaangalia maeneo hayo.

“Nimeona athari ya mvua kwenye eneo la Kariakoo na Rwamlimi na kwa haraka nakwenda kuangalia ufumbuzi kwa kushirikiana na wataalamu wa Tarura”

“Tukisema tusubili bajeti ya fedha za Tarura tutahalibikiwa zaidi hivyo kwa haraka tutaangaika tuweze kusaidia eneo hili” alisema.

Wananchi wanaoishi na kufanya biashara eneo la Kariakoo wamemshukuru mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi ya kuchimba mitaro hiyo kwa wakati.

Wamesema maji ya mvua yamekuwa ni kero eneo hilo hivyo kuchimbwa kwa mitaro hiyo itakwenda kuwasaidia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!