Na Magrethy Katengu
BANDARI ya Dar es Salaam katika kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 2023 imefanikiwa kufanya huduma zaidi ya malengo yake ambapo imehudumia takribani meli 979 kati ya meli 792 na kuhudumia abiria takribani milioni 1 kati ya 900,000, makasha 990,000 kati ya lengo la kuhudumia makasha 500,000, huku mizigo ikiwa ni tani milioni 17.2 kati ya tani milioni 15.6 zilizokusudiwa.
Ameyasema hayo Januari 9,2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mbossa katka Mkutano waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali katika ofisi za TPA ulioongozwa na kauli mbiu inayosema Vyombo vya Habari ni Daraja la Mawasiliano Kati ya TPA, Wateja, Wadau na Umma.
Aidha Bw. Mbossa amesema kuwa kutokana na maboresho ya bandari meli hadi 12 zinahudumiwa kwa wakati mmoja, hivyo kupelekea wastani wa meli 100 kuhudumiwa kwa mwezi mmoja, kutoka meli 70 ndani ya mwezi mmoja lakini
Ameeleza kuwa, kutokana na mikakati mbalimbali ya serikali ya kukuza uchumi wa nchi kumepelekea kuwepo kwa ujenzi wa miradi mbalimbali na hivyo kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha mizigo inayopita katika bandari hiyo.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) imesema kutokana na maboresho na mikakati inayofanywa na Serikali kumefanikisha kuongezeka maradufu kwa meli za mizigo katika bandari mbalimbali zilizopo nchini hususan katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa bandari akizungumzia changamoto inayoikabili bandari ya Dar es salaam amesema miundombinu iliyopo haijitoshelezi kwani ikija meli kubwa moja inalazimika kuhudumiwa na magati mawili hivyo kupitia uwekezaji unaokwenda kufanyika changamoto zinakwenda kutatuliwa na biashara kuongezeka