Home Kitaifa MUWASA YAAGIZA MABOMBA KUKAMILISHA USAMBAZAJI MAJI JIMBO LA MUSOMA MJINI

MUWASA YAAGIZA MABOMBA KUKAMILISHA USAMBAZAJI MAJI JIMBO LA MUSOMA MJINI

Na Shomari Binda-Musoma

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) imeagiza mabomba kukamilisha usambazaji maji kwa asilimia 100 jimbo LA Musoma mjini.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Afisa Mahusiano wa mamlaka hiyo Chausiku Joseph wakati akijibu maswali ya wananchi wa mtaa wa Bweri Bukoba manispaa ya Musoma.

Akijibu mbele ya mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo aliyekuwa akizungumza na wananchi hao amesema tayari mabomba yameagizwa ili usambazaji uendelee.

Amesema eneo la Bweri Bukoba wapo wananchi ambao wameshafikishiwa huduma ya maji na maeneo mengine yanasubiliwa mabomba kufika.

Chausiku amesema kwa sasa mitaa yote 73 katika jimbo la Musoma mjini mtandao wa maji umefika na huduma ya kuwaunganishia wananchi inaendelea.

Afisa huyo wa mahusiano amesema wananchi ambao hawana gharama za kuunganisha maji wanayo nafasi ya kuunganishiwa kwa mkopo.

Amesema kupitia ofisi za serikali za mtaa zipo fomu ambazo zina maelezo namna ya kuunganishiwa maji kwa mkopo na kulipa taratibu.

Akizungumza na wananchi wa mtaa huo wa Bweri Bukoba mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema MUWASA inaendelea kufanya kazi nzuri ili kila mwananchi awe na huduma ya maji kwenye mji wake.

Amesema kama ilivyoelezwa fursa ya kuunganishiwa maji kwa mkopo ipo hivyo mabomba yakifika wananchi wachangamkie kuunganishiwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!