Home Biashara TANZANIA YAJA NA MKAKATI WA KUWA KITOVU CHA UONGEZAJI THAMANI MADINI KWA...

TANZANIA YAJA NA MKAKATI WA KUWA KITOVU CHA UONGEZAJI THAMANI MADINI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema Tanzania imedhamiria kuwa kitovu cha uchenjuaji na uongezeaji thamani madini kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati ili kuongeza fursa za Ajira na Mapato kutoka na mnyororo wa thamani kwenye sekta ya Madini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri Mavunde Jijini Riyadh,Saud Arabia wakati akichangia kwenye mkutano mkubwa wa madini wenye madhumuni ya kujadili nafasi ya madini katika maendeleo ya nchi wazalishaji wa madini.

Waziri Mavunde ameeleza juu ya hatua ambazo serikali inaendelea kuchukua kupitia mapitio ya sera na sheria juu ya kuweka msisitizo kwenye uongezwaji wa thamani ya madini yanayozalishwa nchini.

“ Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara wa kusimamia uongezaji thamani madini ili kutoa fursa kwa watanzania wengi zaidi kunufaika kupitia mnyororo wa thamani wa madini.

Kwa muelekeo wa sasa wa uzalishaji wa nishati safi,madini mkakati ndio yenye uhitaji kwa sasa duniani na Tanzania imebarikiwa kuwa na madini hayo kwa wingi.

Mkakati wa sasa wa Tanzania kupitia sera na sheria zetu ni kuona madini haya yanaongezwa thamani nchini,hii itaifanya Tanzania kuwa kati ya maeneo machache barani Afrika yatakayosimamia uongezwaji thamani wa madini mkakati.

Mradi wa Kabanga Nickel-Ngara, mkoani Kagera unaomilikiwakwa ubia kati ya serikali na wabia ni mfano wa mkakati wa serikali katika kuhamasisha uongezaji thamani nchini Tanzania,kwa kuwa kutajengwa mradi wa kisasa wa kusafisha madini (Multi-metals facility) ya nickel na madini mengineyo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambao utatumia Teknolojia ya kisasa ya Hydromet ili kutosafirisha madini hayo yakiwa ghafi na hivyo kusaidia nchi kupata mapato zaidi,Ajira kuongezeka na kukua kwa teknolojia kutokana na usafishaji huo”Alisema Mavunde

Mkutano huu wa siku tatu ambao unashirikisha mawaziri wa madini kutoka zaidi ya nchi 70 duniani umefunguliwa na Waziri wa Viwanda na Madini wa Saud Arabia Mh. Bandar Alkhorayef

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!