Mkurugenzi wa kanda Tigo Zantel, Aziz Said Ali, akimuelezea Mfanyabiashara wa Mwani, Bwn. Jaha Haji Khamis kuhusu huduma ya Mjasiriamali box katika maonesho ya 10 ya kibiashara Zanzibar,ambapo Tigo zantel ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo.
Na Mwandishi Wetu.
Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo – Zantel imedhamini Maonesho ya 10 ya Biashara yanayoendelea Visiwani Zanzibar Tangu Juzi Januari , 07 na yanatarajiwa kumalizika Januari , 19 , 2024.
Maonesho haya yameandaliwa na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar kwa lengo la kuwapa Fursa wananchi na Wafanyabiashara wa Ndani na nje ya nchi kuzitangaza Biashara zao.
Tigo Zantel kama mdhamini Mkuu wa Maonesho haya amekuja na huduma mbalimbali za Kidigitali , nakusihi tembelea banda la Tigo kujionea.