TASAF wameanza mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea maafisa Ugani kuhusu uendeshaji wa Warsha za jamii,ufanisi wa malipo,masharti ya elimu/afya na majukumu ya kamati za usimamizi.
Akiongea mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi ndugu CPA Chacha Nyamrimba ametoa msisitizo kwa maafisa ugani hao kuwa wanatakiwa waonyesha mabadiliko katika utekelezaji mara baada ya mafunzo haya hasa katika eneo la masuala ya malipo ili kuepuka usumbufu wakati wa ukaguzi.
Nae Mwezeshaji wa Mafunzo haya ndugu Stella Komba ambae pia ni Afisa ufuatiliaji na ushauri wa TASAF Kigamboni akitoa mafunzo hayo amesema awamu ya tatu ya Mpango wa TASAF Kwa kipindi hiki cha pili umejitanua zaidi ambapo utrkelezaji utafanyika Kwa halmashauri zote 184 Tanzania bara na Unguja,Pemba na Zanzibar.
Akizungumzia msisitizo wa kipindi hiki cha pili cha utekelezaji amesema pamoja na mengine msisitizo umewekwa pia katika kuwawezesha walengwa wa TASAF kuongeza kipato na kuwapatia kazi za muda na kkuongeza rasilimali zalishi na kuongeza vitega uchumi.
Akiongelea kuhusu sehemu kuu mbili za mpango huu amesema mpango utajikita kwenye program za jamii zitakazojumuisha miradi ya kutoa ajira Kwa walengwa,kukuza uchumi wa Kaya na uhawilishaji fedha Kwa kuwapa ruzuku.
Pia amewataka maafisa ugani kwenda kutoa elimu na kuwasimamia vyema walengwa ili kufikia malengo tarajiwa.
Kwa Kipindi hiki cha pili TASAF inatarajia kuwafikia Kaya 1,450,000 za walengwa.
Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa TASAF Manispaa ya Kigamboni Bi. Matilda Mwita amewashukuru TASAF Kwa kuleta mafunzo haya muhimu katika kuongeza weledi,ufanisi na uadilifu katika kutekeleza Mpango wa tatu wa TASAF katika kipindi cha pili.