Na Theophilida Felician Kagera.
Kamati ya uongozi wa mtaa wa NHC Kata ya Rwamishenye Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera umewahakikishia wananchi kuzitumia mbinu mbalimbali ili kuvikabili vitendo vya wizi wa mali zawananchi mtaani humo.
Akitoa kauli hiyo Mwenyekiti wa mtaa huo Devid Dominick akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa huo amesema kuwa kutokana na kukithiri kwa vitendo vya watu wanaoshiriki uhalifu wa wa wizi kwa wananchi wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanapambana navyo kwa kila njia.
Amesema kwamba suala la wizi limekuwa tishio na kuwaathiri wakazi wa mtaa akiwemo yeye mwenyewe ambaye ameibiwa mara kadhaa na kuuliwa mke wake mwaka jana 2023 nyumbani kwake.
Amefafanua na kusema kuwa kutokana na hali hiyo wamekuwa wakikabiliana na tatizo hilo kwa kuunda vikosi kazi vya ulinzi shirikishi ambavyo kwa kiasi vimesaidia kwa namna moja au nyingine.
Ameeleza kwamba kwa sasa wameunda kikundi cha vijana 12 waliohitimu mafunzo Jeshi la hakiba (MG) ambao watafanya ulinzi maeneo ya wananchi kwakujitolea huku wakichangiwa Sh 1000 kwa kila mwezi kutoka kwa wananchi kwa ajili yakuwawezesha walinzi hao kufanya kazi ya ulinzi kwa mazingira rafiki.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti amezungumzia juu ya kupambana na vijana wavuta madawa ya kulevya aina ya bangi eneo la shule ya msingi Rwemishasha ambapo ametoa onyo kali kwa wa husika kuacha tabia hiyo mara moja kwani uongozi wa mtaa kwakushirikiana na jeshi la Polisi wako imara watahakikisha watu hao wanadhibitiwa ipasavyo kuvuta bangi eneo la shule hiyo.
“Katika hali ya mapambano siyo mchezo lolote la weza kutokea kwahiyo mimi nasema na simama na Mwenyezi Mungu ntaendelea kupambania wananchi katika hili hatutakubali kuendeleza uhalifu siogopi tutapambana tuu, vijana wangu tusiongope watu waendelee kuvuta bangi kwenye taasisi niwe kimya haiwezikani! haiwezikani! wananchi niungeni mkono muone ntakachokifanya mimi niko tayari kwa lolote bahati nzuri tunavyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vinatuunga mkono kweli kweli” ameeleza wazi Mwenyekiti Devidi.
Hata hivyo amehimiza wenye nyumba hususani nyumba za kupangisha kufanya orodha ya watu wanaowapangisha kwenyenye nyumba zao na orodha hiyo kukabidhiwa kwa uongozi wa mtaa, yote hiyo ikiwa ni sehemu ya kuutokomeza wizi.
Mwenyekiti huyo amehitimisha akipongeza juhudi za Serikali kwa namna inavyoendelea kuleta fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika mtaa huo na kata nzima ya Rwamishenye.
“Rais wetu Mama Samia tunakushukuru sana mama kwakuweza kutuongoza vizuri na kutupatia miradi mbalimbali watanzania tunaimani na wewe, vile vile nipende kumpongeza kijana wetu mchapa kazi Mhe Mbunge wajimbo letu Steven Byabato kwa namna anavyo chapa kazi tunakushukuru sana bila kumsahau diwani pamoja na viongozi wenzangu wamtaa” maneno yake Mwenyekiti Devidi akihitimisha hotuba yake.
Kwa upande wake Yudi Alex Mkaguzi wa Jeshi la Polisi kata Kagondo kwaniaba ya Mkuu wa Polisi wilaya ya Bukoba akihudhuria mkutano huo katika kukazia suala la ulinzi na usalama amesema kuwa ili kuutokomeza wizi ni lazima wananchi wenyewe wawe mstali wambele kutoa ushirikiano wa kuwabaini watu wanaohusika na vitendo hivyo bila ushirikiano wizi utaendelea kuwepo.
Yudi amevitaja baadhi ya vyanzo vya wizi kuwa ni baadhi ya watu kutokupenda kuwajibika kufanya kazi, ulevi, kugoma kuchangia ulinzi na mengineyo.
“Mtu mwingine toka asubuhi yeye ni kunywa pombe tuu yaani anakunywa pombe tuu hela anatoa wapi? vihi unaweza kunywa pombe bila hela? ukiona mtu wahivyo ni mwizi anatumia watu wengine kwenda kuiba, jambo jingine wapo watu wanaopinga suala la ulinzi ukiona mtu wahivyo jua naye ni wakala wa wezi kupitia hadhara hii watu tufanye kazi pia tuwe pamoja katika ulinzi Polisi kama Polisi hatuwezi kukaa kila eneo la mtu jukumu la ulinzi nila kila mwananchi tumeelewana ndugu zangu” amesema Mkaguzi wa polisi Yudi Alex.
Pia amegusia changamoto ya kuwepo kwa watoto chokolaa wanaosababisha usumbufu wa kuwaibia wananchi hivyo ametoa wito akiwasisitiza wazazi na walezi kuwajibika kuwalea watoto wao ili kuepusha adha hiyo vinginevyo watoto watakaokamwatwa wakishiriki matukio hayo watawajibishwa wazazi na walezi wao.
Kadharika amekumbushia wananchi kuwa wepesi katika kujitokeza kutoa ushahidi mahakamani pindi anapokuwa amekamatwa muhalifu ili atiwe hatiani na akabiliwe na mkono wa sheria zaidi kwani bila ushahidi itakuwa ngumu kuwa dhibiti wahalifu.
Nao wananchi wamepongeza juhudi za uongozi huo wa mtaa kwakujitoa na kuendeleza mapambano dhidi ya wizi ambapo mwananchi Jaziru Yassin Ndyetabula akitoa pongezi zake amelalamikia kuachiwa huru kwa watu wanaokamatwa mara kadhaa kwa kufanya vitendo vya wizi.
Jaziru ameliomba Jeshi la polisi kutokuwaachia kiurahisi watu wanamna hiyo kwani wanapokamatwa nakuachiwa inawaongezea nguvu wezi katika kuendelea kuwaibia wananchi.
Imani Sudi Husein ni katibu wa UVCCM kata ya Rwamishenye akiungana na wananchi amewapongeza viongozi wa mtaa wa NHC kwa jinsi unavyoendelea kutekeleza mambo mbalimbali ya maendeleo kupitia ilani ya CCM ambapo ameahidi kwamba chama kitaendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa uongozi huo ili kuongeza bidii ya kuchapa kazi sawa sawa ya kuwatumikia wananchi huku naye akipongeza juhudi za Rais na Mbunge Mhe Steven Byabato kwa jinsi ambavyo amekuwa mpambanaji toka kuingia madarani mwaka 2020 hadi sasa kwani mambo yanaendelea vizuri na kwa kasi kila kona ya Jimbo.