Januari 4, 2024 Christina Latin Mrua Mkazi wa Salasala Dar Es Salaam amekabidhiwa rasmi zawadi yake ya Vifaa vya nyumbani kutoka HISENSE ambavyo ni TV, Microwave, Sub Woofer na Friji kutoka kampeni ya MAGIFTI DABO DABO inayoendelea hivi sasa , Christina alimchagua kaka yake kuwa Mshindi mwenza katika promosheni ambaye naye amekabidhiwa Vifaa hivyohivyo ili kuleta maana halisi ya Kampeni MAGIFTI DABO DABO.
Meneja wa Tigo Kanda ya Kinondoni kaskazini Bwn. Shedrack Mutalemwa akikabidhi zawadi za Vifaa vya Ndani ambavyo ni Friji , Microwave , Subwoofer , Sound bar , na TV mshindi wa Magifti Dabo Dabo kutokea Salasala Jijini Dar Es Salaam , Katikati ni Neema Nyagonde, Meneja Mauzo Tigo Kanda ya Ubungo
Ikumbukwe Kampeni hii inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo ilizinduliwa Mwishoni mwa Mwezi Novemba Mwaka jana huku ikimtambulisha Haji Manara kama SEMAJI la Kampeni hii, ambapo mteja wa Tigo anaweza kushinda Fedha Taslimu hadi Milioni 10, Safari ya Kwenda Dubai au Zanzibar, Set ya Vifaa vya Ndani ambavyo ni Sound bar, Friji, TV na Microwave na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) , kingine kinachovutia katika kampeni hii ni kwamba ukishinda kitu kimoja wapo kati ya ivyo unamchagua na yeyote umpendae ili apewe zawadi iyoiyo uliyoshinda hii ndio maana halisi ya MAGIFTI DABO DABO.
Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa ivyo kwa mshindi , Meneja wa Tigo Kanda ya Kinondoni kaskazini Bwn. Shedrack Mutalemwa amewasisitiza wakazi wa Salasala na Watanzania kwa ujumla kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa ili kuibuka washindi maana kampeni bado inaendelea
” Mwezi Disemba Tigo tuliwapeleka washindi 15 DUBAI , na wengine walienda Zanzibar katika kampeni hii hii” wapo pia waliojishindia Pesa Taslimu na wapo pia wamejishindia Vifaa vya Hisense kama dada yetu Christina mnayemuona mbele yenu, kwahyo kampeni bado inaendelea fanyeni miamala na TIGO PESA kwa wingi, Lipa kwa Simu, nunua vifurushi ili utengeneze mazingira ya kuibuka Mshindi ” amesema Mutalemwa
Akizungumza kwa furaha kubwa baada ya kupokea Set mbili ya Vifaa vya ndani kutoka HISENSE Mshindi Christina amesema kwakweli haamini macho yake kama tukio lililokua linafanyika ni la kwelii,
” Mara ya kwanza napigiwa simu kuambiwa nimeshinda Vifaa vya nyumbani vya Hisense katika kampeni ya MAGIFTI DABO DABO sikuamini kwakweli, Nilijua ni utapeli lakini baadae nkaja kuamini baada ya kuona kumbe nimepigiwa na namba 100 nawasihi Watanzania tumieni Tigo, fanyeni miamala maana ndo Siri ya Ushindi, Amesema Christina kwa furaha kubwa.