Home Kitaifa TCCIA KUMSAIDIA RAIS SAMIA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA KUPITIA SEKTA BINAFSI

TCCIA KUMSAIDIA RAIS SAMIA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA KUPITIA SEKTA BINAFSI

-SALAMU ZA MWAKA MPYA ALIZOTOA ZAWAGUSA

Na Shomari Binda-Musoma

CHEMBA ya Biashara,Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) imeahidi kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kukuza uchumi wa taifa kupitia sekta binafsi.

Ili kufikia malengo ya kukuza uchumi kutoka asilimia 8 ya mwaka 2023 hadi asilimia 20 kwa mwaka huu wa 2024 ni ushirikiano wa karibu wa sekta binafsi na serikali.

Kauli hiyo imetolewa na kaimu Rais wa TCCIA na Makamu wa Rais upande wa biashara Boniphace Ndengo kwa niaba ya Rais wa chemba Vicent Minja.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Musoma wakati wa kutoa salamu kwa Rais Samia za wafanyabiashara na wadau wa sekta binafsi amesema chemba Ipo tayari kuisaidia serikali.

Ndengo amesema sekta binafsi inachochea masuala ya uwekezaji wa wafanyabiashara wakubwa na kuwafanya kuwekeza Tanzania katika shughuli za kiuchumi.

Anesema uwekezaji ukifanyika unakuza uchumi wa nchi na kufanya mambo mengine ya serikali kuendelea kufanyika.

Makamu wa Rais huyo wa TCCIA amemuhakikishia Rais Samia wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati ili serikali iweze kutekeleza miradi ya kuwahudumia wananchi.

Amesema pasipo kulipa kodi kwa wakati ni kushindwa kutekeleza wajibu hivyo TCCIA itaendelea kuwahimiza wafanyabiashara kutambua umuhomu wa kulipa kodi.

“Tunamshukuru mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan namna anavyotekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo”

“TCCIA kama chemba ya wafanyabiashara tunahaidi kumpa ushirikiano wote ili kuhakikisha malengo kusudiwa ya taifa yanafikiwa” amesema Ndengo

Amesema katika salamu za mwaka mpya wakati akilihutubia taifa ipo mipango na maelekezo kama muongozo uliotolewa na Rais Samia ambao unapaswa kufuatwa.

“Kwa niaba ya Rais wa TCCIA na wafanyabiashara wote tunaahidi tena kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia ili kufikisha taifa mahala sahihi”, ameongeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!