Home Kitaifa MUHONGO: UFUGAJI WA SAMAKI KWA NJIA YA VIZIMBA UTAONDOA UMASIKINI KWA JAMII...

MUHONGO: UFUGAJI WA SAMAKI KWA NJIA YA VIZIMBA UTAONDOA UMASIKINI KWA JAMII ZETU

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo amesema ufungaji wa samaki kwa njia ya vizimba ni njia pekee ya kuondoa umasikini.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Etaro alipokuwa kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa maabara kwenye sekondari ya Etaro amesema wananchi walio kando ya ziwa wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo.

Amesema serikari inatoa mikopo ya vifaa vya uvuvi wa vizimba pamoja na boti za kisasa lakini wananchi wa Musoma vijijini bado kwa asilimia kubwa hawajajitokeza kuomba mikopo hiyo.

Muhongo amesema hali hiyo inamsikitisha hasa pale anapoangalia wanaoomba mikopo hiyo wengi wanatoka nje ya mkoa wa Mara na wamekuwa wakinufaika nayo.

Amesema wananchi wanapaswa kutuma maombi na kuacha kulalamika hali ngumu wakati fursa za kupata fedha zipo.

“Niwaambie ndugu zangu wa hapa Etaro na jimbo zima la Musoma vijijini tuchangamkie fursa ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba”

“Aina hii ya ufugaji wa samaki ndio utatutoa kwenye umasikini na serikali inatoa mikopo ya vifaa na boti naomba tuchangamkie fursa hii” amesema Muhongo.

Amesema maafisa uvuvi wapo tayari kuelekeza namna ya kuomba mikopo hiyo na kuwataka kuunda vikundi ili kupata mikopo hiyo.

Wananchi wa Etaro wameomba maafisa uvuvi kuwatembelea na kuwaelekeza namna ya kujiunga na namna ya kuomba mikopo hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!