Home Kitaifa HAKUNA MBADHILIFU WA MIRADI YA MAENDELEO ATAKAYEACHWA KUCHUKULIWA HATUA”RC MTANDA”

HAKUNA MBADHILIFU WA MIRADI YA MAENDELEO ATAKAYEACHWA KUCHUKULIWA HATUA”RC MTANDA”

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Said Mtanda amesema hakuna mbadhilifu wa fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo ambaye hataachwa kuchukuliwa hatua.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa ( RCC ) kilichofanyika kwenye ukumbi wa uwekezaji wa mkoa.

Amesema serikali chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imekuwa ikileta fedha nyingi kwaajili ya miradi ya maendeleo na lazima umakini wa usimamizi uwepo.

Mtanda amesema kama fedha zinakuja kwaajili ya mradi zitumike kama zilivyolengwa kwenye maeneo husika.

Amesema kama mkuu wa mkoa hatomvumilia yoyote na hatosita kumchukulia hatua na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ambaye atakwenda kinyume na usimamizi wa miradi ya maendeleo.

Hakuna hatua kali ambazo hazitaacha kuchukuliwa kwa yoyote atakayefanya ubadhilifu kwa fedha zinazotolewa na serikali kwenye miradi ya maendeleo.

Watumishi wote wanaosimamia miradi ya maendeleo wasimamie kwa umakini na kila mradi thamani ya fedha ionekane”,amesema Mtanda.

Katika kuelekea mwaka mpya wa masomo mwaka 2024 mkuu huyo wa mkoa amewataka wakuu wa wilaya kusimamia uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali na msingi na kila mwenye umri wa kuandikishwa aandikishwe.

Amesema kwa wanafunzi wote waliohitimu elimu ya msingi na kupata nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari watapata nafasi ya kuendelea kwa kuwa yapo madarasa ya kutosha na sekondari mpya.

Aidha katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho cha ushauri ya mkoa amesisitiza suala la ukusanyaji wa mapato kwa kuwa yanasaidia serikali kuzirejesha kwaajili ya shughuli za maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!