Na Mwandishi Wetu.
Shule ya Awali na Msingi ya LUSAJO iliyopo Mbondole Ilala Jijini Dar Es Salaam, Desemba 16 , 2023 ilifanya hafla fupi ya kuwapongeza wanafunzi wake, ambao wamehitimu masomo ya Awali na kuingia Elimu msingi, Hafla iliyoudhuriwa ni viongozi mbalimbali wa Kiserikali, Kidini, Wazazi na wananchi wanaoizunguka shule hiyo.
Akizungumza baada ya hafla iyo Mwenyekiti wa Bodi Lusajo Nursery & Primary School Bwn. Geofrey Msukwa alisema , Wameamua kuwekeza katika Elimu ili kuwajengea watoto uwezo wa kufanya mambo makubwa katika umri mdogo
” Lusajo Nursery and Primary School ni Shule Mpya kwa maana imesajiliwa mwaka huu , lakini ukiangalia ni Shule inayofanya vizuri kitaaluma Kwa mfano katika Ukanda huu ni Shule itakayokuwa tishio , Leo tumeona watoto walivyoandaliwa vizuri na walimu kupitia michezo ya kitaaluma na Maigizo mbalimbali yaliyotuonesha hapa na tumeona pia wana uwezo mku wa wa kujielezea kwa Lugha ya Kiingereza hilo ni Jambo la Kujivunia sana , Nitumie nafasi hii kuwaalika Wazazi wanaofikiria ni Shule ipi bora ya kumpeleka mtoto jibu ni LUSAJO NURSERY & PRIMARY SCHOOL iliyopo Mbondole Ilala , Jijini Dar Es Salaam pia kwa Mawasiliano ni kupitia simu Namba 0784660949 “
Naye kwa Upande wake Mkuu wa Shule hiyo Bwn. Owden Ndile alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazozifanya kuboresha Sekta ya Elimu Nchini pamoja na Kuruhusu wawekezaji Binafsi kuwekeza katika Elimu.