Home Kitaifa Tawi jipya la Tigo shop lazinduliwa Buswelu

Tawi jipya la Tigo shop lazinduliwa Buswelu

Na Neema Kandoro Mwanza

Tawi jipya la kutoa huduma za tigo katika Kata ya Buswelu limezinduliwa kwa lengo la kusogeza huduma ya kukopesha simu janja.

Akizungumza Jana kwenye eneo hilo Diwani wa Kata hiyo Sarah Ng’hwani alisema anawapongeza tigo kwa kufungua tawi hilo kwani ilikuwa ni kilio cha wananchi walio wengi hivyo wao kama Serikali wanaunga mkono kusogeza huduma hiyo.

Mkurugezi Mtendaji wa tigo Robert Sanyagi alisema Ufunguzi huo umeambatana na ofa kabambe za bei ya chini kwa simu.

Aliwataka Wana Mwanza waunge Mkono juhudi zinazofanywa na Selikali Makini ya Mama Samia Suluhu Hassani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!