Home Kitaifa WANANCHI WATAKIWA KUJIRIDHISHA KABLA YA KUNUNUA ARDHI

WANANCHI WATAKIWA KUJIRIDHISHA KABLA YA KUNUNUA ARDHI

Na Shomari Binda – Musoma

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Slaa amewataka wananchi kujiridhisha kabla ya kuchukua uamuzi wa kutoa pesa kufanya ununuzi wa ardhi.

Pamoja na rai hiyo Kwa wananchi wataalam wa ardhi nao wametakiwa kuwasaidia wanapo wafikia ili wasijiingize kwenye migogoro na kutapeliwa.

Waziri Jerry Slaa ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na maafisa ardhi na viongozi wa mkoa wa Mara kwenye ukumbi wa uwekezaji.

Amesema wapo wananchi ambao wanatumia njia za mkato kununua ardhi bila kufuata taratibu na baadae kujiingiza kwenye migogoro.

Slaa amesema licha ya kuibua migogoro wapo ambao wanatapeliwa kwa kuuziwa ardhi ambazo ni za watu wengine na kupoteza fedha kwa njia ya kutapeliwa.

Waziri huyo amewataka wananchi kabla ya kufanya uamuzi wa kununua kujilidhisha kwanza kwa kufika ofisi ya ardhi ambazo zipo kila wilaya na mkoa hapa nchini.

Aidha Waziri huyo amewataka maafisa ardhi kuwasaidia wananchi bila mizunguko pale wanapowafikia kwa lengo la kununua ardhi.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Mara Yahaya Nawanda amesema kile alichokiongea Waziri ni agizo kwa maafi ardhi na kinachotakiwa ni kwenda kufanya utekelezaji.

Amesema kuwasaidia wananchi kuna baraka kubwa hivyo kila mmoja kwenye nafasi yake aende akatekeleze majukumu yake.

Kamishina Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Mara Joseph Batinamani amesema wamepokea kile kilichozungumzwa na Waziri Slaa na wanakwenda kukifanyia kazi.

Amesema mkoa wa Mara bado unaemdelea na kliniki yake wilayani na elimu itaendelea kutolewa kwa wananchi jiu ya masuala ya ardhi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!