Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi wanatarajia kurejea kambini leo Desemba 4 kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Wydad Casablanca Disemba 9
Wydad Casablanca imepoteza mechi mbili za mwanzo katika ligi hiyo ya Mabingwa Barani Afrika ikiwa ni faida kwa Simba Sc ambao wao hawajapoteza mechi yoyote.
“Wydad imepoteza mechi mbili za mwanzo lakini hiii haitupi nafasi ya kwenda kichwa kichwa kwani Wydad ni sawa na Mnyama mkali aliyesinzia huwezi jua ataamka saa ngapi na ataamkia kwa nani?!!
Sisi tunapaswa kujiandaa tukiamini tunakwenda kucheza na mpinzani mgumu tukimkuta bado amelala fresh tunapita nae tukimkuta ameamka tunakomaa nae” alisema Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally.