Na Magrethy Katengu
Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Maendeleo ya Taifa utakaofanyika Desemba 9, 2023 katika Ukumbi wa Julius Nyerere(JNCC) Rais Dkt Samia Suluhu Hassani ataufungua rasmi.
Akizungumza leo Jijini Dar es saalam Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema lengo kuu la Mkutano huo ni kuzindua ,kupokea na kujadili taarifa ya kitafiti ya Tathimini ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na mafanikio yaliyopatikana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa dira hiyo iliyoanza kutekelezwa tangu mwaka 2000 na itafikia mwisho 2025,
Sanjari na hayo amesema pamoja na mafanikio mengine taarifa ya tathimini inaonyesha kuwa pato la Mtanzania (GDP per capital income limeongezeka kutoka dola za kimarekani 399.5( TZS 322,597) mwaka 2000 hadi kufikia dola za Kimarekani 1200(TZS 2,880,000) mwaka 2022.
“Katika mkutano huu Mheshimiwa Rais atazindua rasmi Timu kuu ya Kitaalam ya Dira (National Vision Core Technical Team) na kamati ya Usimamizi wa dira (National Vision Steering Commitee) pamoja na nyenzo za kidigitali zitakazotumika katika kukusanya maoni ya wadau” amesema Waziri Profesa Mkumbo
Sambamba na hayo amesema Mkutano huo utahudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka pande zote za nchi wadau hao ni pamoja na ikiwemo Viongozi wakuu wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa serikali ya Zanzibar ,Mawaziri ,Makatibu wakuu ,Wakuu wa Mikoa ,Viongozi wa vyama vya siasa, Dini taasisi za serikali na binafsi na Viongozi wa Makundi mbalimbali ikiwemo Wazee,watu wenye ulemavu,wakulima,wafugaji,wavuvi,na wachimbaji wa madini, wasomi na waandishi wa habari ambapo jumla.yake ni wadau 971 watashiriki
Aidha Tanzania imefikia asilimia 124 ya kujitosheleza kwa chakula ikilinganishwa na lengo la kufikia asilimia 140 ifikapo mwaka 2025 kwani hii ni hatua imewezesha Tanzania kukabiliana na njaa kwa mikoa na wilaya zote nchini kuwa na mazingira mazuri ikiwemo Mtandao wa barabara za lami na zege (paved road) katika mikoa umeongezeka kutoka Km 4,179 mwaka 2000 hadi Km 11,966.38 mwaka 2023 huku idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi vikipungua kutoka vifo 760 kwa vizazi hai 100,000 mwaka 2000 hadi kufikia vifo 104 mwaka 2022 ikiwa tumevuka lengo la kufikia vifo 265 ifikapo 2025.
Aidha Wananchi wanambwa na kusisitizwa kufuatilia mchakato wa kuandaa Dira mpya na kushirikia kikamilifu katika kitoa maoni yao kuhusu Tanzania waitakayo katika miaka ijayo