Home Michezo FIFA NA TFF ZAIFUNGIA KLABU YA SIMBA KUFANYA USAJILI

FIFA NA TFF ZAIFUNGIA KLABU YA SIMBA KUFANYA USAJILI

Klabu ya ligi kuu nchini Tanzania Simba Sc imefungiwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu FIFA kufanya usajili wa wachezaji wa kimataifa kutokana na madai ya klabu ya Teungueth ya nchini Senegal kutoa madai kuhusu mauzo ya Mchezaji Pape Ousmane Sakho kabla ya kujiunga na Simba.

Hii leo Novemba 23, 2023 kupitia mtandao wa X (zamani Twitter) wa TFF wametoa taarifa inayosema kuwa amuzi huo umefanywa baada ya klabu hiyo kushinda kesi ya madai dhidi ya Klabu ya Simba.

Simba ilitakiwa iwe imetekeleza uamuzi huo ulipotolewa ndani ya siku 45, lakini haikufanya hivyo.

Wakati FIFA imechukua uamuzi wa kuifungia Simba kufanya usajili wa wachezaji kimataifa, pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia Klabu ya Simba kufanya usajili wa ndani.

Sakho ambaye kwa sasa anachezea timu ya Quevilly Rouen Metropole ya Ufaransa akitokea Klabu ya Simba

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!