Home Kitaifa CCM MKOA WA MTWARA YAPONGEZA JITIHADA ZA OFISI YA WAZIRI MKUU KUKABILIANA...

CCM MKOA WA MTWARA YAPONGEZA JITIHADA ZA OFISI YA WAZIRI MKUU KUKABILIANA NA MAAFA

NA. MWANDISHI WETU
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara, Mussa saidi nyengedi amepongeza juhudi za Ofisi ya Waziri Mkuu katika masuala ya menejimenti ya maafa kwa namna inavyoyaratibu nchini.

Ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ayeshughulikia masuala yua Sera, Bunge na Uratibu Mhe Ummy Nderiananga alipotembelea ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoani humo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa hatua zinazochukuliwa kuzuia na kujiandaa kukabiliana na maafa kwa kamati ya usimamizi wa maafa mkoa wa huo.


Alipongeza hatua ya ofisi hiyo ya kuzijengea uwezo Kamati za Maafa kwa kuzingatia umuhimu wa elimu ya maafa kwani itasaidia kuendelea kujiandaa na kukabiliana na Maafa endapo yatatokea.

Aidha alitumia fursa hiyo kuendelea kukumbusha jamii kujiandaa kuliko kusubiri maafa yanatokea ndipo zichukuliwe hatua.
“Mmefanya vizuri sana kuja Mkoani kwetu kutupa elimu ya masuala haya ya majanga na maafa, ni vyema jamii ikawa na utayari wa kukabili endapo maafa yanatokea, nakushukuru kipekee Naibu Waziri kwa namna mnavyoratibu masuala haya ambayo yapo katika Ilani yetu ya Chama chetu,”Alisema Nyengedi

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe Ummy Nderiananga akieleza lengo la ziara yake alisema Ofisi yake imeona umuhimu wa kuendelea kuzijengea uwezo Kamati za Maafa nchini kwa kuzingatia taarifa za Tahadhari za uwepo wa mvua za El nino zilizotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ambapo ilielezwa zitaathiri mikoa kumi na nne ikiwemo Mtwara .


Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Mwanahamisi Mukunda alisema Wilaya yake itayatumia mafunzo hayo kwa tija na mafanikio makubwa huku akishukuru Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa namna ilivyoendelea kuifikia jamii kwa kutoa elimu ya masuala ya menejimenti ya maafa.

=MWISHO=

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!