Kiasi cha shilingi milioni 30 pamoja na magari mawili mapya yatatolewa.
DAR ES SALAAM, TANZANIA, Tarehe 22 Novemba 2023 – Kampuni ya mtindo wa maisha ya kidigitali inayoongoza Tanzania, Tigo, ina shauku kutanganza uzinduzi wa kampeni yake mpya ya ‘Magifti Dabo Dabo’. Kampeni hii imeandaliwa kwaajili ya kusherehekea wateja wetu wote kwa malengo waliyoweza kuyakamilisha mwaka huu pamoja na kuwazawadia kwa uaminifu wao kwa kuwapatia wao na wapendwa wao zawadi zenye kusambaza upendo katika kipindi hiki cha sikukuu.
Kampeni ya ‘Magifti Dabo Dabo’ itafanyika kwa siku 80, ikitumia msingi wa kampeni ya ‘Cha Wote’ ambayo ilikuwa inalenga katika kuhamasisha wateja kudumisha mtindo wa maisha ya kidigitali wakati huo huo ikiwa inawahamasisha kufanya tathmini ya malengo yao ya nusu mwaka. Kampeni hiyo vile vile iliwazawadia wateja zawadi za fedha taslimu kama hamasa ya kuendela kufuatilia malengo yao waliojiwekea. Kwa hiyo, katika msimu huu wa sikukuu, tunataka kusherehekea pamoja na wateja wetu kwa kila walicho fanikiwa pamoja na kufikisha zawadi hizo kwa wapendwa wao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Bi Angelica Pesha alisema, “Nina furaha kubwa kutambulisha kampeni yetu ya ‘Magifti Dabo Dabo’ ambayo ni kama uthibitisho wa utayari wetu katika kushukuru uaminifu wa wateja wetu. Kampeni hii inadhihirisha hamu yetu ya kuwapatia wateja wetu sio tu bidhaa na huduma za kipekee bali pia kumbukumbu ya kudumu na fursa ya wateja wetu kusherehekea wakati tukiwa tunawawezesha kuonyesha furaha yao na wale wawapendao katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu. Tunaamini sio tu kwamba kampeni ya ‘Magifti Dabo Dabo’ itaimarisha muunganiko wetu na wateja wetu lakini pia itafanya sherehe za wateja wetu kuwa za kipekee na hatimaye kuleta matokeo chanya wakati huu wa furaha.”
Msingi wa kampeni ni kwamba, sio tu kwamba mshindi anashinda, lakini pia wana fursa ya pekee ya kuchagua mtu mmoja maalum wa kupokea tuzo kama hiyo, hivyo Magifti Dabo Dabo. Sasa, hiyo ni dozi mara mbili ya furaha! Zawadi za Magifti Dabo Dabo sio zawadi za kawaida, zina anzia katika bonasi ya papo kwa hapo, vifaa vya nyumbani vya kiwango cha juu (Friji, TV, Microwave na Soundbar) zawadi za pesa taslimu hadi milioni 30, safari za kulizolipiwa gharama zote kwenda Zanzibar na Dubai, pamoja na magari mawili mapya kabisa.
Akisisitiza kuhusu tamaduni ya Tigo katika misimu ya sikukuu, Mkurugenzi wa Masoko kutoka Tigo, Edwardina Mgendi amesema,”Msimu wa sikukuu hutoa fursa nzuri ya kutoa shukrani zetu kwa wateja wetu. Ishara hii inawahimiza kuendelea kutumia huduma za Tigo, na kuthibitisha imani yao na upendeleo wao katika huduma zetu. Kwa kusherehekea wateja wetu kufikia malengo yao ya mwaka huu na kuwapa nafasi ya kushinda zawadi wanazoweza kufurahia na wapendwa wao tunachangia katika kukuza hamasa ya sherehe na kusaidia kuunda uzoefu usioweza kusahaulika.”
Wateja wataingia katika droo za zawadi za kila siku, kila wiki, mwezi pamoja na zawadi kuu kwa kila muamala unaofanywa kupitia Tigo Pesa na kwa bando lolote lililonunuliwa katika kipindi cha kampeni. Kadiri wateja wanavyofanya miamala mingi, ndivyo nafasi zao za kushinda zinavyoongezeka. Vile vile, wateja wa Tigo pia wana uhakika wa kujishindia bonasi za papo hapo za hadi dakika 35 (on-net) na SMS 25 wanaponunua vifurushi kuanzia Tshs 500 kupitia Tigo Pesa, Tigo Rusha, au muda wa maongezi.
Ili kupata nafasi ya kujishindia Magifti Dabo Dabo na kusherehekea mafanikio yako pamoja na mpendwa wako piga *150*01# kwa miamala yako yote ukitumia Tigo Pesa na kununua vifurushi piga *147*00# au tembelea wakala wa Tigo Rusha aliye karibu nawe.