Home Kitaifa MUWASA, RUWASA WAENDELEZA KASI YA USAMBAZAJI MAJI YA BOMBA JIMBO LA MUSOMA...

MUWASA, RUWASA WAENDELEZA KASI YA USAMBAZAJI MAJI YA BOMBA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma ( MUWASA) na Mamlaka ya Usambazaji Maji Mjini na Vijijini (RUWASA) wameendeleza kasi ya usambazaji maji jimbo la Musoma vijijini.

Usamvazaji wa maji hayo ni kutoka ziwa victoria ambapo miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa na mamlaka hizo.

Kazi za BADEA zinaendelea ambapo bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama mradi wa shilingi bilioni 70.5 wenye kuzalisha lita 17.5 milioni za maji unafanyika.

Maji ya bomba hili yatasambazwa Musoma Vijijini Kata za Mugango, Tegeruka, Busambara, Kiriba na Ifulifu) ambapo vifaa vya kukamilisha mradi kutoka Uturuki na China vimeanza kuwasili nchini

Kazi za MUWASA Kata ya Tegeruka: Vijiji vya Tegeruka, Mayani na Kataryo vimetandaziwa mabomba kazi hii ya utandazaji mabomba ni endelevu.

Kijiji cha Mkirira kimefikishiwa maji ya bomba kutoka ziwa victoria na wananchi wameanza kuyatumia na kufurahia.

Vijiji vya Nyegina na Kurukerege vinakamilishiwa miundombinu ya kupata maji ya bomba

MUWASA inasambaza pia maji ya bomba kwenye Kata 4 (Etaro, Nyegina, Nyakatende & Ifulifu) za Musoma Vijijini kutoka kwenye chanzo chake cha maji kilichoko Bukanga, Musoma Mjini

Kwa upande wa kazi za RUWASA Maji ya Chumwi, Mabuimerafuru tenki lenye ujazo wa lita 300,000 limejengwa kijijini Mabuimerafuru ambapo yatasambazwa kwenda vijiji vya Mabuimerafuru, Chumwi, Masinono na Bugwema

Mradi wa maji ya Kata ya Bwasi; tenki la ujazo wa lita 150,000 limejengwa kijijini Bwasi huku maji ya tenki hili yatasambazwa Vijiji vya Bwasi, Kome na Bugunda ambapo chanzo cha maji ya Kata ya Bwasi ni maji ya bomba la Bujaga/Bulinga

Kata ya Murangi; Tenda imeishatolewa kwa kupata mabomba ya kusambazia maji kwenye Kata hiyo yenye vijiji vya Lyasembe na Murangi yatatoka kwenye tenki la Mabuimerafuru.

Miradi ya Kata za Busambara na Kiriba matangazo ya kumtafuta Mkandarasi yametolewa ili mradi huo uweze kuanza mara moja.

Vijiji vyote 68 vina miradi ya maji ya bomba kutoka ziwa victoria na utekelezaji wake uko kwenye hatua mbalimbali.

Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospter Muhongo amesema taarifa za utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa maji ya bomba vijijini zitaendelea kutolewa.

Amesema wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuishukuru serikali chini ya uongozi mzuri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za usambazaji wa maji safi na salama vijijini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!