Na Shomari Binda-Bunda
MCHEZAJI wa zamani wa timu ya Yanga na Taifa Stars Edibily Jonas Lunyamira ametoa ushauri kwa wachezaji walioshiriki mashindano ya Ryakitimbo Cup 2023 wilayani Bunda.
Ushauri uliotolewa na mchezaji huyo ambaye alitamba miaka ya 90 hadi 2000 ni kuhakikisha wanatunza vipaji vyao na kuzingatia maelekezo ya makocha.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa fainali ya mashindano hayo kati ya Kambubu na Mugeta fc amesema mchezo wa soka kwa sasa ni ajira kubws kwa wanao zingatia.
Amesema wachezaji wanaocheza leo ni tofauti na kipindi chao nakudai leo mchezaji kwa kipaji chake anasajiliwa kwa mabilioni ya fedha.
Lunyamra amesema kwa kulinda vipaji vyao wanatakiwa kuachana na starehe zilizopitiliza na kuzingatia maelekezo ya walimu.
Mchezaji huyo amempongeza muandaji wa mashindano hayo Moses Ryakitimbp kwa kuwa amefanya jambo kubwa kuandaa mashindano yaliyoshirikisha timu zaidi ya 40 zikiwemo za watoto chini ya miaka 15 na wanawake.
Amesema ameona vipaji vingi kupitia mashindano hayo ambavyo vinapaswa kulindwa na sio kuachwa vikapotea.
Kwa upande wake muandaji wa mashindano hayo Moses Ryakitimbo amesema amekusudia kuendesha Ryakitimbo Cup kwa miaka 5 mfulululizo.
Amesema yeye ni mpenzi wa michezo na hataacha vipaji vinavyopatikana kupitia mashindano hayo vipotee bali vitakuwa vikiendelezwa.
Muandaaji huyo amesema timu ya wachezaji bora waliopatikana watakwenda jijini Dar es salam kucheza na mabingwa wa Ndondo Cup timu ya Madenge.
Kwenye mchezo wa fainali hiyo timu ya Mugeta fc wameibuka mabingwa kwa kuifungab timu ya Kambubu bao 1-0 na kuibuka na kitita cha shilingi milioni 2 kikombe pamoja na medali huku mshindi wa pili akipata zawadi ya shilingi milioni moja.