Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mariam Mwinyi ameendelea na ziara yake nchini Uingereza inayolenga kutamatisha ukatii na udhalilishaji wa kijinsia
Ziara hiyo ya kikazi iliyoendelea jana tarehe 17 Novemba 2023.
Mama Mariam Mwinyi amekutana na Taasisi ya Big Win inayoongozwa na Dk .Kasete Admasu wenye ofisi zao Uingereza katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Mazungumzo yao wamegusia ushirikiano katika kufanya kazi kwa pamoja eneo la program itakayohusisha ukuaji wa mtoto hususani kinga na ulinzi dhidi ya udhalilishaji wa kijinsia kwa kuwawekea mazingira salama, pamoja na kuimarisha lishe kwa maendeleo ya ukuaji.