Home Kitaifa SERIKALI YAPONGEZA KAMPENI YA UPANDAJI MITI YA SHIRIKA LA Vi-AGROFORESTRY

SERIKALI YAPONGEZA KAMPENI YA UPANDAJI MITI YA SHIRIKA LA Vi-AGROFORESTRY

Na Shomari Binda-Musoma

SERIKALI imepongeza kampeni ya upandaji miti inayoendeshwa na shirika la Vi-Agrofotestry katika kupambana na uhifadhi wa mazingira.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Musoma Ally Mwendwa katika zoezi la upandaji miti zaidi ya 470 katika shule mpya ya msingi Bweri Bukoba.

Zoezi hilo limeendeshwa ikiwa ni siku ya 2 ya maonyesho ya kilimo mseto yanayofanyika katika kituo cha mafunzo Bweri yanayoendana na miaka 40 ya shirika hilo katika kufanya shughuli zake.

Akizumgumza mara baada ya zoezi la upandaji miti Katibu Tawala huyo amesema miti ni rafiki wa binadamu na wanyama hivyo kupanda miti na kuitunza ni jambo la muhimu.

Mwendwa amelipongeza shirika hilo na kudai linafanya kazi kubwa kwa kushitikiana na serikali ili kufikia malengo ya kutunza na kuhifadhi mazingira.

Mwenyekiti wa kamati ya maonyesho hayo Rashid Bakari amesema katika kipindi hiki cha maonyesho wamepanda miti zaidi ya laki 8 kwenye maeneo mbalimbali.

Amesema katika kampeni ya upandaji miti kwa sasa wanazalisha miti kwaajili ya kuigawa kwa wananchi na taasisi mbalimbali.

Mwenyekiti wa mtaa wa Bweri Bukoba Richard Bendera amesema kwa kushirikiana na wananchi na wanafunzi wameahidi kuitunza miti hiyo ili iweze kukua.

Amesema miti ya matunda,kimvuli,mbao na kuni iliyopandwa iwapo itakua itakuwa msaada mkubwa shuleni hapo pamoja na wananchi wa mtaa wa Bweri Bukoba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!