Na Theophilida Felician, Kagera
Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera imeendelea na juhudi za utekelezaji wa mkataba wa usimamizi wa shughuli za lishe.
Yamebainika hayo kwenye kikao cha kamati ya lishe kilichofanyika hii leo Tarehe 15 Novemba ukumbi wa Halmashauri
hiyo.
Afisa lishe wilaya Janeth Mahona akiwasilisha taarifa ya tathimini ya mkataba wa shughuli hizo kwa niaba ya Mkuu wa divisheni ya afya ustawi wa jamii na lishe amebainisha kuwa Halmashauri ya Bukoba imekuwa ikijikita zaidi katika kutekeleza shughuli mbalimbali za lishe ambapo katika utangulizi Afisa huyo ameanza kwakueleza kuwa lishe bora ni muhimu katika ukuaji wa mtoto tangu akiwa tumboni hadi anapofikisha umri wa miaka 5.
Amefafanua malengo ya mkataba wa usimamizi wa shughuli za lishe kuwa ni
Kuongeza uwajibakaji na usimamizi wa shughuli za lishe katika ngazi ya jamii, Suala la lishe kulipa kipaumbele katika ngazi ya jamiii na katoa fursa sawa za kupambana na utapiamlo na udumavu.
_ kuhakikisha jamii kupitia viongozi wao kwa pamoja wanashiriki ipasavyo katika kupanga, kutekeleza na kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa kazi za lishe na malezi ya watoto.
-Kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika kupanga, kutekeleza na kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa afua zalishe.
-Kufanikisha uboreshaji wa hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo kwa jamii.
Taarifa hiyo imeeleza wazi tathimini ya utekelezaji kwa kila kiashiria kwa mwezi Aprili- Juni na Julai- Septemba mwaka 2023
Viashiria hivyo ni kiwango cha vikao vya kamati za maendeleo ya kata vilifanyika na kujadili agenda za lishe na kuwasilisha taarifa kwa wakati 100% kwa 100%, kiwango cha vijiji vilivyofanya maadhimisho ya siku ya afya na lishe ya vijiji 100% kwa 100%, kiwango cha vijiji vilivyobandika taarifa za lishe kwenye mbao za matangazo ya vijiji 100% kwa 100%, kiwango cha kaya zenye watoto chini ya miaka 5 na wajawazito walitembelewa na wahudumu wa afya ngazi ya jamii na kupewa elimu ya lishe 81.66% kwa 66.5%, vijiji vilivyotunga na kutekeleza sheria ndogo ndogo juu ya masuala ya lishe 100% kwa 100%, watoto chini ya miezi 6- 59 waliobainika kuwa na utapiamlo mkali ni 0.2% kwa 0.1% na nyingine kadha wa kadha.
Aidha kata 28 kati ya kata 29 sawa na 96.5% zimetekeleza mpango wa utoaji chakula shule zote kwa 100% tofauti . kata 1 ya Kyaitoke sawa na 3.4% iliyotekeleza mpango huo kwa 83.3%
Wajawazito waliohudhuria hudhurio la kwanza katika vituo vya kutolea huduma za afya katika kata 29 ni 71.9% ikilinganishwa na 76.1% ya Aprili – Juni.
Aidha 0.1% ya watoto waliobainika kuwa na utapiamlo mkali kutoka katika kata 4 za Butelankuzi, Ibwela, Katoro na Kibirizi ikilinganishwa na 0.2 ya watoto waliobainika kuwa na utapiamlo mkali kata 6 za katoro, Kyaitoke, Ruhunga,Kishanje, Kibirizi na Butelankuzi katika kipindi cha Aprili- Juni ambapo kata hizo nne sawa na 13.8% watoto waliobainika kuwa na utapiamlo mkali walipewa Rufaa ya kwenda kutibiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Licha ya mafanikio Janeth pia amezitaja changamoto katika utekelezaji wa mkataba wa shughuli za lishe ambazo ni ufanisi wa utekelezaji wa mkataba wa usimamizi wa afua za lishe ngazi ya jamii kupungua 94% Aprili- Juni hadi 90.8% Julai Septemba, baadhi ya kata hazitoi taarifa za shule binafsi katika kata zao, wanafunzi wengi bado hawapati mlo shuleni, na kiwango cha kaya zenye wajawazito na watoto chini ya miaka 5 zilizotembelewa kimeshuka kutoka 81.8% hadi 66.5%
Ameongeza kwamba Mkoa Kagera ni miongoni mwa mikoa yenye watoto wengi wa chini ya miaka 5 wenye udumavu wanaokadiriwa kufikia 34.4% .
Afisa huyo akihitimisha wasilisho la taarifa hiyo ameishukuru na kuipongeza timu nzima kwa kuwajibika pamoja na kufanikiwa yote hayo huku akitoa wito wa kuwasisitiza kuendelea kupambana hatimaye kuutokomeza kabisa udumavu na utapiamlo kwa jamii.
Mkuu wa wilaya Bukoba Mhe. Erasto Sima akishiriki kikao hicho ameipongeza Halmashauri hiyo chini ya Mkurugenzi wake Bi Fatina Laay kwa namna inavyoonyesha juhudi katika utekelezaji wa afua zalishe kwa wananchi.
“Hii ni hatua nzuri naona tunaenda kwa takwimu zipo zilizoshuka tunashukuru nyingi zimepanda hatutaki zishuke tupambane tuzipandishe na hizi zilizoshuka jitahidini kuwajibika katika majukumu yenu kama ilivyo hivi kwa masuala ya lishe tatueni kero za wananchi watendaji wa kata ninakuja huko kuzisikiriza kero za wananchi sitokubali kuona jambo linahalibika mtu ukiwepo kila mmoja awajibike kwa nafasi yake Mhe Rais amekuwa akisisitiza suala la kuwajibika na sisi lazima tuwasisitize hilo tushirikiane itatusaidia” Amesema Mkuu wa wilaya Erasto Sima
Mihtasari ya vikao mbalimbali vya lishe ambavyo vimekuwa vikifanyika katika Halmashuri hiyo vimesomwa wazi mbele wajumbe na Mwandishi wa vikao Erasmus Evaristo.
Kikao hicho kimehudhuriwa na watu tofauti tofauti miongoni mwao wakiwa watendaji wa kata, waganga wafawidhi na wakuu wa idara.