Home Kitaifa VIJANA WA CCM NA UWT WAMETAKIWA KUENDELEZA AMANI NA MSHIKAMANO ULIOPO KATI...

VIJANA WA CCM NA UWT WAMETAKIWA KUENDELEZA AMANI NA MSHIKAMANO ULIOPO KATI YA TANZANIA NA CHINA

Na Scolastica Msewa, Kibaha
Katibu wa Nec Siasa na uhusiano wa kimataifa SUKI Rabia Abdallah Hamid amewataka vijana viongozi wa CCM kuendeleza amani maelewano na mshikamano uliopo kati ya Tanzania na Chama tawala cha kikomunisty cha nchini China CPC kwa maslahi mapana ya Chama na jumuhia zake ikiwa ni pamoja na Maendeleo ya Nchi kwa ujumla.

RABIA ametoa Wito huo wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo Vijana 50 wa UWT na UVCCM katika masuala mbalimbali ya uongozi wa kisiasa yaliyowezeshwa na Chama Cha Kikomunist Cha China CPC huko Kibaha mkoani Pwani katika Shule ya uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere Kibaha kwa Mfipa.

Amesema Chama Cha Mapinduzi kina
matarajio makubwa baada ya mafunzo hayo ya siku kumi kwamba utendaji na uongozi wa viongozi hao wa UVCCM na UWT utakuwa bora na wa mfano katika maeneo mbalimbali ya nchini yetu.

“Nitoe rai kwenu kuendeleza roho ya amani, maelewano na mshikamano, pia kuwa sehemu ya kuchagiza mahusiano tuliyonayo na vyama rafiki
ikiwemo CPC, ikikumbukwa kwamba Umoja wetu ni nguvu”
amesema Rabia.

“Ndugu Wahitimu, katika kipindi cha siku kumi mlizokaa hapa, nafahamu mmejifunza mada zinazohusu; Uongozi wa kisiasa: Mpango wa Maendeleo Ulimwenguni, Mpango wa Usalama Ulimwenguni, Mpango wa Ustaarabu wa Kimataifa, Utekelezaji wa dhana mpya ya maendeleo na maendeleo ya hali ya juu, Maslahi ya kitaifa, utaifa, Misingi ya Itikadi kuu katika ulimwengu”

“Mada zingine mlizosoma ni Uongozi na usimamizi wa Kitaifa wa Kimkakati wa Mabadiliko ya Kijamii na Kiuchumi, Mazungumzo ya hadhara, mawasiliano, uhusiano wa vyombo vya habari na Chama kutengeneza taswira, Utawala, Maadili, na Uwajibikaji katika uongozi wa kisiasa, pamoja na Jitihada za kupunguza umaskini”

“Ninawapongeze kwa kushiriki kikamilifu na hatimaye kuhitimu mafunzo haya muhimu kwa Chama na taifa kwa ujumla” amesema Rabia.

“Niwashukuru wataalam kwa utayari na kutumia muda wenu kubadilishana uzoefu miongoni mwetu maana Uimara wa Chama Cha Mapinduzi unatokana na kuamini misingi ya UTU, UJAMAA na Kujitegemea”

“Ibara ya nne ya katiba ya CCM imeeleza wazi mani ya Chama chetu ya kwamba Binaadamu wote ni sawa na kila mtu anastahili heshima ya kutambuiwa na kuthaminiwa utu wake sambamba na Ujamaa na Kujitegemea ndio njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru hivyobasi, kwa misingi na Imani hizo ndio Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika hotuba yake ya kustaafu Uenyekiti wa Chama
Chetu Agosti 1990, katika ukumbi wa Diamond Jubilee alisema, “…bila ya CCM madhubuti, nchi yetu itayumba”

”Kutokana na CCM kuendelea kusimamia misingi hiyo, ndio pale ilipopelekea nguvu zake na kujitoa kwa kila namna ili kusaidia na vyama vyengine vya ukombozi kwa nchi jirani katika kugombea uhuru wa nchi zao, na kwa misingi hiyo hiyo vyama hivyo vimebaki kua imara pia” amesema Rabia.

“Ninaamini na ni matumaini yangu kwamba, mliitumia nafasi hii kujifunza kwa mazingatio makubwa na kubadilishana uzoefu wa kiutendaji, uongozi na changamoto zake na jinsi mlivozitatu katika maeneo yenu, muhimu wa kushiba itikadi na dhana ya uzalendo kwa nchi yetu, pamoja na kutambua umuhimu wa elimu na mafunzo kwa wanachama ili muende kushusha taaluma mlizozipata huko mnakosimamia” amesema.

“CCM pia inaamini kwamba kupitia mafunzo haya yaliyowaleta pamoja kwa takriban siku 10 sasa,
mmeweza kujenga na kuboresha mshikamano na umojamiongoni mwenu ambao utadumu kwa manufaa ya chama”

Mkuu wa Shule ya Uongozi Prof. Marcelina Chijoliga amewashukuru CPC kwa kuwezesha mafunzo Vijana ambao wanaonekana wameiva katika kutumikia Chama.

Aidha Prof. Chijoliga aliomba uongozi wa CPC kuendelea kufadhili Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa uongozi kwa CCM na jumuhia zake kwa lengo la kufanikisha chagua mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa kitengo Cha mawasiliano ya kimataifa Cha CPC, YU HAIILIN amesema mafunzo hayo yamedumisha urafiki mkubwa na mahusiano kwa washiriki hai huku akiahidi kuwaalika nchini china Viongozi hao ili waweze kwenda kujifunza masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani Mwinshehe Shaban Mlao amesema makundi ya vijana na wanawake ni tegemeo kubwa katika upatikanaji ushindi wa ccm hivyo amewaka vijana hao Kwenda kuwafundisha vijana wengine wenzao elimu waliyoipata katika Mafunzo hayo ya siku kumi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!