Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo ameendelea kuhamasisha uchangiaji wa ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi katika shule za sekondari .
Kwa sasa ujenzi umeanza wa maabara kwenye shule ya sekondari Mtiro ambayo wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma kwenye shule hiyo wamehamasika kuwa na maabara.
Mtiro Sekondari ilifunguliwa Mwaka 2006 iliyoko Musoma Vijijini ni ya Kata ya Bukumi yenye vijiji vinne, ambavyo ni Bukumi, Buira, Buraga na Busekera.
Mbunge Muhongo, ameendelea kushawishi na kuhimiza wananchi kushirikiana na serikali kuharakisha ujenzi na uboreshaji wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye kila sekondari iliyoko Musoma Vijijini.
Maabara hizo no za masomo ya Fizikia, Kemia na Bailojia ambayo yamekuwa yakitoa nafasi kubwa ya ajira.
Akizungumzi shule hiyo ya Mtiro sekondari Muhongo amesema haina maabara hata moja kwa hiyo wanafunzi wake hawavutiwi kuchagua kusoma masomo ya sayansi.
Amesema vile vile ufaulu wa masomo ya sayansi ni mdogo hivyo jitihada zinahitajika ili maabara hizo ziweze kupatikana kwenye shule hiyo.
Muhongo amesema mwaka 2022 wanafunzi 139 walimaliza kidato cha nne ambapo mwanafunzi mmoja (1) ndiye alienda kidato cha tano kusoma masomo ya sayansi
Amesemaa mwaka huu wa 2023
wanafunzi watakaomaliza kidato cha nne ni 123
ambapo wanafunzi wanaosoma fizikia ni 21
wanafunzi wanaosoma kemia ni 26
“Tumeamua kujenga maabara tatu za masomo ya sayansi huku michango ujenzi imeanza kutolewa kama ifuatavyo”
“Michango kutoka kwa wananchi shilingi 7,989,100,michango kutoka kwa walimu na wanafunzi usombaji wa maji, moramu na mawe vyenye thamani ya shilingi 3,640,000, mbunge wa jimbo amechangi saruji mifuko 125,mfuko wa jimbo umechangia saruji mifuko 200 na nondo 29”, amesema
Amesema Mtiro sekondari inaomba mchango kwa kuchangia moja kwa moja kupitia akaunti ya benki ya shule ya Mtiro sekonsari ya NMB kwa namba 30301200299
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa mchango wako utakaoipatia Mtiro Sekondari.