Na Shomari Binda-Musoma
MDAU wa maendeleo wa jimbo la Musoma vijijini amechangia vitanda viwili vya kisasa kwaajili ya huduma kwa wagonjwa
Vitanda hivyo vimetolewa kwenye hospital ya halmashauri ya (Musoma DC) yenye hadhi ya hospital ya Wilaya inayowahudumia wananchi wa jimbo hilo.
Mdau huyo ambae ni mzaliwa wa Musoma Vijijini na daktari bingwa ambae ameomba kwa sasa asitajwe jina lake.
Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amemshukuru mdau huyo kwa kuchangia huduma za jamii.
Amesema vitanda hivyo vitasaidia kupatiwa huduma wananchi wanapofika kwenye hospital hiyo kwaajili ya kupatiwa matibabu.
Muhongo amesema wadau wa kuchangia maendeleo kwenye jamii wanapokelewa na kushukuliwa kwa kile wanachokitoa.
Ameeema hospital hiyo mpya imejengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero Kijijini cha Suguti na imeanza kutoa huduma za afya za aina mbalimbali.
Vifaa tiba muhimu vilivyoko hositalini hapo ni pamoja na Digital X-Ray, Ultrasound, Oxygen plant
(Oxygen inatengezwa hospitalini hapo na kupelekwa kwa bomba (pipe) wodini.
Wadau wengine wameendelea kuombwa kujitokeza kuchangia shughuli za maendeleo kwenye sekta mbalimbali katika jimbo la Musoma vijijini.