Na Theophilida Felician, Kagera
Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera itaendelea kuwahimiza wazazi na walezi wa watoto kushiriki suala la kuchangia chakula cha watoto shuleni kama yalivyomaekezo ya Serikali.
Hayo yamebainishwa kwenye kikao cha kamati ya lishe cha kujadili utekelezaji wa afua zalishe kwa kipindi cha robo tatu ya Julai – Septemba 2023 na mpango kazi wa Oktoba- Desemba ambapo taarifa ya Divesheni ya elimu ya wali na msingi ikiwasilishwa na kaimu idara ya elimu msingi Joseph Matope imeyataja mafanikio yake na changamoto ikiwemo ya baadhi ya wana jamii kuwa wagumu kukubali kuchangia chakula ipasavyo shuleni.
Mkurugenzi wa Halmashauri Fatna Laay akiwa Mwenyekiti wakikao na wenzake daada ya kupokea taarifa hiyo nakuijadili kwa kina nakuzitaja changamoto zinazopelekea watoto wengi kutokupata chakula wawapo shuleni imempelekea Mkurugenzi huyo kumuagiza kaimu elimu ya msingi kuwaandikia barua wazazi nawalezi juu yakuwa taarifu yakwamba ifikapo mwezi Januari kila mzazi na mlezi atimize wajibu wake wakuwachangia watoto chakula shuleni jambo ambalo litasaidia watoto wote kupata chakula kuliko ilivyo kwa sasa.
Amefafanua kuwa suala la chakula shuleni ni muhimu kwa watoto katika kuwajenga kiafya na kuongeza ufaulu zaidi.
Ameongeza kwamba elimu zaidi iendelee kutolewa kwajamii kutoka kwa watalaamu ili changamoto hiyo ya baadhi ya watu kuzembea kuchangia chakula isiendelee kujitokeza kwani kufanya hivyo nikuwanyima haki ya msingi watoto.
Awali akitoa taarifa hiyo ya emu ya awali na msingi kaimu Joseph amesema kuwa Divisheni hiyo imetekeleza shughuli za lishe kwa kuhamasisha kutoa elimu kupitia mashamba darasa, uhamasishaji wa elimu ya kujitegemea pamoja na usafi wa mazingira na unawaji mikono.
“Shughuli zote hizi zililenga katika kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni nawanajikinga na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kuambukiza” Ameeleza Joseph Matope.
Hata hivyo amesema shughuli hizo zilitekelezwa katika shule 154 katika hizo 141 zikiwa za serikali na 13 zikiwa za binafsi ambazo zina jumlaya wanafunzi 80604 wavulana wakiwa ni 40572 na wasichana 40032.
Amesema kuwa shughuli za lishe zinatekelezwa ili kuboresha afya za wanafunzi, kupunguza utoro na kuongeza ufaulu wa wanafunzi huku akisisitiza kuwa shabaha yao ni kuongeza ufaulu kutoka 85% hadi 97% ifikapo Juni, mwaka wa 2024, nakupunguza utoro kutoka 15% hadi 5%
Kwa upande wake Afisa lishe wa Halmashauri hiyo Donald Kalenzo ameeleza kuwa katika jitihada za utekezaji wa shughuli zalishe pia wanajumuisha na utekelezaji wa mpango jumuishi wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto unaowalenga watoto kuanzia umri wamiaka 0 hadi 8, hivyo ametoa wito akiwasihi watalaamu, watendaji na viongozi kutoa ushirikiano wapamoja kwa malengo ya kufanikiwa zaidi juhudi hizo.
Katika kikao hicho idara mbalimbali zimewasilisha taarifa zautekelezaji wa shughuli zalishe ambazo ni Idara ya maendeleo ya jamii, kilimo, mifugo, na uvuvi, na elimu.
Katika jitihada za utekelezaji wa afua zalishe Halmashauri hiyo imeendelea kuunga juhudi hizo kwakutoa fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji washughuli hizo za lishe hiyo ikiwa ni mwendelezo wa kupambana na utapiamlo na udumavu kwa watoto.