NA Mwadishi wetu
KATIKA Kuadhimisha siku ya miji duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Oktoba 31 tangu kuwnzishwa kwake 2014, Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mtaa Tanzania ( TALGWU) kimesema kuwa haki za Wafanyakazi ni haki za binadamu.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Octoba 31 2023 Katibu wa Chama hicho, Rashid Mtima Amesema ieleweke kwamba haki za wafanyakazi ni sehemu ya muhimu ya ukuaji endelevu na jumuishi wa miji hapa nchini na duniani kote.
Amesema mafanikio yanayopatikana katika ukuaji wa miji unachagizwa na utendaji kazi bora wa wafanyakazi waliopo katika sekta mbalimbali wakiwa na jukumu la kuhakikisha eneo la kazi linakuwa salama bila manung’uniko na kulipa umuhimu suala la haki watendaji hao.
“TALGWU inatambua kazi inayofanyika katika miji hapa nchini hasa usimamizi wa miundombinu ya barabara, usafi wa mazingira, utunzaji wa taka ngumu na maji pamoja na shughuli zote za Maendeleo zinazo lenga kukuza miji hapa nchini zinazofanywa na watumishi wa Umma ambao ni wanachama wetu.”
Amesem kuwa TALGWU inatambua jukumu hilo na wanahitaji wafanyakazi wanafanya kazi katika mazingira bora ba salama huku wakipatiwa hazi za msingi ambazo zitawaongezea ari na morali ya kufanya kazi kwa ubora.
Mtima amesema kuwa siku ya Miji duniani hutumika kama fursa ya kukuza nia ya Jumuiya ya Kimataifa katika ukuaji wa miji duniani, kusukuma mbele ushirikiano kati ya nchi katika kushughulikia changamoto za ukuaji wa miji na kuchangia maendeleo endelevu ya miji duniani kote.
Hata hivyo chama hicho kinapenda kitoa ujumbe wa waajiri wa serikali za Mtaa nchini(Mameya na Wakurugenzi ) kuwa ” haki za wafanyakazi ni haki za binadamu na ni sehemu ya ukuaji na jumuishi miji
Aidhs anewapongeza wanachama kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhamikisha eanasimamia ipasavyo suala la mipango miji kushughulikiea changamoto za ukuajim miji