Home Kitaifa MBUNGE MATHAYO AOMBA FEDHA UBORESHAJI KITUO CHA AFYA BWERI

MBUNGE MATHAYO AOMBA FEDHA UBORESHAJI KITUO CHA AFYA BWERI

Na Shomari Binda

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ameiomba serikali fedha kwaajili ya uboreshaji wa kituo cha afya Bweri.

Maombi hayo ameyaelekeza kwenye Ofisi ya Raid Tamisemi wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni hii leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu

Wakifatilia kikao cha kwanza cha bunge la 12 la mkutano wa13 wananchi wa Kata ya Bweri wamemshukuru mbunge wa jimbo la Musoms mjini Vedastus Mathayo kwa kuomba fedha serikalini kwaajili ya kituo chao cha afya.

Wamesema kituo hicho kina umuhimu mkubwa hivyo kinahitaji maboresho ili kiweze kutoa huduma zikiwemo za kulazwa na huduma nyingine.

Wananchi hao wamedai eneo la Bweri lina wakazi wengi wanaokitumia kituo hicho hivyo kinahitaji vifaa tiba pamoja wataalamu wa kuwahudumia.

Mmoja wa wananchi wa Kata hiyo Bweri Athuman Kitwara amesema mbunge Mathayo kuomba fedha serikarini kupitia Tamisemi ili kukiboresha anajua umuhimu wake.

Amesema afya ni suala la msingi na pale mwananchi anapokuwa na afya njema anaweza kufanya shughuli za kiuchumi.

“Kituo hiki kina umuhimu mkubwa na kinawahudumia watu wengi tunamshukuru mbunge Mathayo kuomba fedha kwaajili ya maboresho” amesema Kitwara.

Kwa upande wake Amiri Juma amesema kituo cha afya Bweri ni cha muda mrefu na kinahitaji kuongezwa majengo na vifaa tiba ili kiendelee kutoa huduma.

Leo katika kikao hicho cha kwanza cha mkutano wa 13 wa bunge la 12 mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo aliuliza swali la nyongeza kwenye Wizara ya Tamisemi ni lini itapeleka fedha kwaajili ya kituo cha afya Bweri kwaajili ya maboresho ya kituo hicho.

Akijibu swali la mbunge huyo Naibu Waziri Tamisemi Dkt. Festo Dugange amesema kituo hicho ni cha kimkakati na serikali itatenga fedha kwaajili ya kituo hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!