Home Kitaifa KAMPENI YA MASTABATA YAZIDI KUSHIKA KASI, MIL. 350 KUTOLEWA KILA WIKI

KAMPENI YA MASTABATA YAZIDI KUSHIKA KASI, MIL. 350 KUTOLEWA KILA WIKI

BENKI ya NMB imeendelea kutangaza neema kwa wateja wake ambapo kupitia kampeni ya mpya ya  Mastabata Halipoi itaweza kugawa zawadi kemkem sambamba na safari za kwenda Zanzibar na Afrika Kusini hii ikiwa ni kwa wateja wote watakaokuwa wakifanya miamala yao kupiti kadi au kwa njia ya mtandao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya Mastabata Halipoi iliyofanyika mkoani Tanga mkuu wa kitengo cha Kadi kutoka NMB   Filbert Casmir alisema kuwa zimetengwa fedha tasilimu jumla ya Shilingi Million 350 ambazo zitatoka kila wiki kwa wateja 100 kila mmoja akiondoka na kitita cha laki laki moja (100, 000) na endapo mteja atakutwa na mtoa huduma akifanya malipo ya bidhaa kupitia kadi yake ya Benki papa hapo atazawadiwa shilingi  elfu hamsini (50, 000).

Alisema hatua hiyo ni njia moja wapo ya NMB kurudisha  mapato yake kwa jamii ambapo pia wamekuwa wakichangia huduma mbalimbali zikiwemo sekta  za elimu na afya  huku akiwataka na kuwahamasisha watanzania kuachana na mayumizi ya fedha tathlimu kwaajili ya usalama zaidi.

“Kupitia kampeni hii ya Mastabata Halipoi tunaendelea kuhamasisha malipo kwa kutumia kadi na kuachana na matumizi ya fedha taslimu,  kupitia kampeni hii tutakuwa na droo ya kila wiki na tumeandaa kiasi cha shilingi million 350 ambazo zitakuwa zikishindaniwa kwa wateja wetu washindi 100,  kila mmoja atashinda pesa taslimu laki 1 lakini tukikukuta unafanya manunuzi kupitia kadi palepale tukupatia shilingi elfu hamsini  tumia simu yako kufanya manunuzi hadi kampeni itakapoisha kwa muda wa miezi mitatu”. 

Aliongeza kuwa mbali na washindi hao ambao watazawadiwa ila wiki kutakuwepo pia na droo ya kila mwezi kila mshindi akiingiziwa  kiasi cha laki tano kwenye akaut yake  na kupewa ofa ya kwenda kutalii Zanzibar sambamba na zawadi ya pamoja kwa  washindi 7 na wenza wao ambao watagharamikiwa safari ya kwenda Afrika Kusini kwa muda wa siku tano wakilipiwa kila kitu na benki hiyo.

“Kwenye droo ya kila mwez tutakuwa na washindi 30 na kila mmoja ataingiziwa kwenye akaunt yake shiling laki tano na pia tutawapeleka Zanzibar na hapa kutakuwa na washindi 10 ambao watakaa huko wakilipiwa kila kitu na benki na zaidi ya hapo tutakuwa na zawadi ya pamoja kwa washindi saba wakiwa na wenzi wao ambao watapelekwa Africa  Kusini kwa jumla ya siku 5  wakilipiwa kila kitu na benki ya NMB Ili kuweza  kushinda zawadi hizi lazima wateja watembee na kadi za NMB kwaajili ya kufanya manunuzi,  kampaeni itaisha january 25, 2024” .alisema Casmir.

Akizindua Kampeni hiyo mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ameipongeza benk ya NMB kwa namna ambavyo wanaendelea kutoa huduma zake kwa jamii ikiwa ni kuchanhia maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo za Afya na elimu hatua ambayo inakwenda kuunga mkono jitihada za serikali katika kuwafikia wananchi.

Aliwataka wananchi kuachana na matumizi ya fedha tathilimu badala yake kuhamia kwenye matumizi ya kidigital njia ambayo ni  salama na inapunguza upotevu wa pesa.

“Niwapongeze sana Benki ya NMB ambao pamoja na kuendelea kuboreaha huduma zenu bado mmekuwa mkijitolea kuunga mkono jitihada za serikali katika sekta kama vile elimu na Afya  mnastahili pongezi”

“Kuendelea kuchangia Uchumi unaokwenda kidigital ni pamoja na kuachana na matumizi ya fedha tathlimu, mbali na usalama wa fedha zako ni bora zaidi kutumia matumizi ya kadi kwa sababu kama nchi tunaingia gharama kubwa kuchapisha fedha  kwahiyo matumizi ya fedha kupitia mitandao ni salama zaidi kwaajili ya malipo” alisema Kindamba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!