Home Kitaifa MAKATIBU WENEZI CCM WATAKIWA KUSEMEA KAZI NZURI INAYOFANYWA NA SERIKALI

MAKATIBU WENEZI CCM WATAKIWA KUSEMEA KAZI NZURI INAYOFANYWA NA SERIKALI

Na Shomari Binda-Musoma

MAKATIBU wa Siasa Itikadi na Uenezi wa CCM mkoa wa Mara wametakiwa kusemea kazi nzuri inayofanywa na setikali.

Kauli hiyo imetolewa na Katobu wa CCM mkoa wa Mara Ibrahim Mjanaheri alipokuwa akifungua kikao kazi na semina kwa makatibu wenezi kutoka wilaya za mkoa wa Mara.

Amesema serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa kwenye miradi mbalimbali ambayo inapaswa kusemewa.

Katibu huyo wa CCM mkoa wa Mara amesema ipo miradi ikiwemo ya elimu, afya maji na mingine ambayo inafanyika kila wilaya ambayo inatekelezwa na serikali katika kuwahudumia wananchi.

Amesema miradi yote inapaswa kuzungumziwa na makatibu wenezi kwa kuwa ndio wenye jukumu la kufanya hivyo kutoka.kwenye chama kinachoongozab serikali.

Katibu huyo wa CCM mkoa wa Mara amesema idara ya uenezi ina umuhimu mkubwa ndani ya chama ikiwa na nafasi ya kuzungumzia yale yanayofanywa na serikali.

Amesema mafunzo yatawajenga makatibu hao wenezi na kwenda kuisemea serikali na kujibu hoja mballmbali zikiwemo za mitandao.

Kwa upande wake Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa mkoa wa Mara Simon Rubugu amesema semina hiyo ina lengo la kuwajengea uwezo Makatibu wenezi katika kutimiza majukumu yao.

Amesema .baada ya mafunzo hayo kwa wenezi watakwenda kufanya kazi ya kuimalisha chama na kukisemea na kujibu hoja mbalimbali zikiwemo za upinzani kwa ufasaha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!