Na Mwandishi wetu
Zaidi ya washiriki 500 kutoka kwa wadau wakuu wa Maendeleo katika sekta ya Asasi za kiraia/Azaki, sekta binafsi, Serikali pamoja na wananchi wanatarajiwa kushiriki katika wiki ya azaki itakayoanza oct 23 hadi 27 mwaka huu jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil society (FCS) Francis Kiwanga amesema lengo la wiki hiyo ni kuzileta pamoja taasisi za kiraia ,watunga sera,wanateknojia pamoja na wadau wengine kubadilishana mawazo
Amesema kuwa, majadiliano ya mkutano huo yatajikita katika ujumishwaji wa teknolojia kwenye kazi za Azaki, kuziwezesha na kuzipa nguvu jamii zilizotengwa,utetezi ushirikiano na uchechemuzi wa digitali,Data takwimu kwa aijili ya kuleta mabadiliko,Teknolojia na maadili ,ubunifu wa teknolojia kwa maendeleo endelevu .
Hata hivyo amesema ufunguzi wa tukio litakuwa na mpangilio wa kuvutia kwani zitawasilishwa changemoto za maendeleo kwa namna ambayo itqchochea tafakuri wiki nzima na kubadilishana maarifa kupata mbinu na mchakato wa usuluhishi wa ufumbuzi wa changamoto za kijamii
.
“Katika wiki ya Azaki tutaangalia wapi tulipotoka, tupo wapi na sasa tunakwenda wapi, mabidiliko ya kidigitali na teknojia yamebadilisha mifumo yetu katika jamii kwa kiasi kikubwa na ina uwezo wa kuendelea kuleta mabadiliko makubwa zaidi” amesema Kiwanga
Aidha, amesema miongoni mwa mada zitakazojadiliwa katika wiki ya azaki ni pamoja na Teknolojia na utetezi wa kijamii, elimu na mafunzo ya digitali nchini Tanzania, matumizi ya takwimu kuleta manufaa kwa jamii pamoja kuimarisha usalama mitandaoni.
Kwa upande wake, Doreen Domic kutoka Stanibic Banki amesema kuwa, wao kama taasisi binafsi ya kifedha wamefurahi kuwa sehemu hiyo ya azaki katika kushiriki kwani mwanzo walikua hawashiriki ipasavyo.
“Sekta binafsi ilikua ikiwekwa mbali lakini kwa sasa stanibic Banki tupo na tunashiriki katika kuleta mabadiliko ya teknolojia”
Naye, Nuria Mshare, Mwakilishi mkazi ambae ni mshauri wa azaki amesema wiki hiyo itawaleta wadau mbalimbali kujadili masuala ya teknolojia inavyosaidia vijana kugeuza kuwa fursa kiuchumi.
Aidha Wiki hiyo itaongozwa na kauli mbu isemayo ‘ teknolojia na jamii yetu ” na Mkutano utafunguliwa na Meya wa Jiji la Arusha mhe Maximilian Matle Iranqe akiambatana na Balozi wa Uswizi Didiet Chassot hivyo anapenda kushiroki ajisajili kupitia tovuti csoweek . or. tz/home