Na Shomari Binda-Tarime
MWENYEKITI wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Mara na mkuu wa mkoa huo Said Mtanda ameonya watu wanaokwamisha uteketezaji wa mashamba ya bangi wakiwemo wanasiasa.
Kauli hiyo ameitoa alipokuws Kijijji cha Nkerege wilayani Tarime akiongoza vikosi vya ulinzi na usalama kuharibu mashamba ya bangi.
Amesema zipo taarifa za uwepo wa watu wanaodaiwa kukwamisha zoezi hilo jambo ambalo serikali haliwezi kuvumiliwa.
Rc Mtanda amesema oparesheni hiyo ni endelevu na hakuna jani la bangi litakalo salia na mkoa wa Mara umejipanga kutekeleza jukumu hilo.
Amesema kwa sasa sheria zimebadilika na adhabu kali zimekuwa zikitolewa kwa wale wanaojihusisha na kilimo na biashara haramu ya bangi.
“Wapo watu wanaotaka kujaribu kukwamisha zoezi hili wakiwemo wanasiasa wasijaribu kufanya hivyo waache zoezi hili liendelee kufanyika”
“Tutahakikisha hakuna jani la bangi litakalosalia na oparesheni hii ni endelevu na wahusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua” amesema Mtanda.
Mkuu huyo wa mkoa amesema wameiomba serikali karuhusu bonde la mto Mara kutumika kwa kilimo kikiwemo cha miwa ili kudhibiti zaidi kilimo cha bangi eneo hilo.
Katika oparesheni hiyo iliyoongozwa na mkuu huyo wa mkoa ekali 800 za mashamba ya bangi ziliteketezwa na watuhumiwa kadhaa kukamatwa kutoka na kujishughulisha na kilimo hicho.