Home Kitaifa JMAT KUSAINIANA MKATABA NA SHIRIKA LA HWPL KATIKA MASUALA YA AMANI YA...

JMAT KUSAINIANA MKATABA NA SHIRIKA LA HWPL KATIKA MASUALA YA AMANI YA DUNIA

Na Magrethya Katengu

Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania(JMAT) imesainiana Mkataba wa kufanya kazi pamoja na Shirika la Kimataifa la Amani lijulikanalo kama Heavenly Culture World Peace restoration of light(HWPL)

Kusaini kataba huo ni katika Mkutano wa Kimataifa uliofanyika jijini Seoul nchini Korea Kusini Agost 17-19 ,2023 uliowahusisha viongozi wa dini na wadau mbalimbali wa Amani kutoka ulimwenguni kote

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Leo Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu JMAT Askofu Dkt Israel Ole-gabriel Maasa juu ya Ziara ya Mwenyekiti JMAT nchini Korea Kusini ,Kenya,na Iran Sheikh Dkt Alhad Mussa , Salum ambapo amesema alipata mwaliko huo ulikuwa na mafanikio mengi kubwa zaidi ni kusaini wa mkataba huo wa mashirikiano ya amani ya dunia

Katika Ziara hiyo mwenyekiti aliambatanana na Bi Fatma Kikkides ambaye Mratibu JMAT Taifa na Ayoub Sanga Mkurugenzi wa idara ya mipango,fedha,uchumi na utekelezaji na jumuiya kupitia wawakilishi hao ilinufaika kwa kukutana na wadau mbalimbali wa amani hivyo kukuza mtandao wa kufanya kazi na watu wengi duniani kwa sjili ya amani ya dunia .

Mahusiano ya kimataifa na tasaasisi HWPL katiks ziara hiyo Korea Mratibu wetu Fatma Kidikkes kapewa ubalozi wa wa amani Duniani kupitis Shirika tanzu la.HWPL linaloahughulikia amani kwa wanawake liitwalo International Women Peace Group(IWPG)’’emesema Katibu..

Samba na hayo amesema Mwenyekiti na timu aliyoambatana nayo walipata fursa ya kutembelea Makumbusho ya vita ya Korea kusini na Kaskszini iliyowahi kutokea mwaka 1950-1953 waliona athari za vita kupata funzo kubwa sana

Pia Mwenyekiti aliendelea na Ziara yake mnamo Septemba 26 ,2023 alienda Jijini Mombasa katika shughuli ya kumtawaza. Mufti Mpya wa Krbya Sheikh Mshali Khamisi Mshali Ashiraazy kupitia taasisi ya Kemnack Nchini Kenya ambapo jambo hilo limeleta heshima kubwa JMAT

.Hata hivyo Mwenyekiti JMAT alipata mualiko wa kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Kiislam na Mahusiano. na. dini mbalimbali Jijini Tehran nchini Iran ambapo mkutano huo ulifunguliwa na Rais wa Iran Mhe Ayotollah Ibrahim ambapo katika mkutano huo Sheikh Dkt Alhad alipata fursa ya kutoa hotuba ya masuala ya umoja wa Kiislam na Din mbalimbali kuzungumza. na vyombo vya habari.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa JMAT $heikh Dkt Alhad Musa amesema Jumuiya hiyo kupitia ziara hiyo wamejifunza mambo mengi sana ambayo nchi hizo zilizopitia machafuko ya vita na kupata athari kubwa sana na wanajutia mpaka Leo waliwaeleza hawataki kusikia kabisa uvunjifu wa amani hivyo Tanzania haina budi kujifunza na kuitunza hii amani iliyopo .

Tuache kabisa magomvi uchochezi tuangalie wenzetu ambao tayari wamefikwa na machafuko tujifunze na kuona kuwa vita ni kitu hatari sana binafsi watanzania nawaasa tivumiliane tuheshimiane tusibaguane na tuendelee kumshukuru sana Mwenyezi Mungu ameendele kutusaidia kutunza tunu ya amani mpaka sasa“‘amesema Sheikh Dkt Alhad

.aliongeza kuwa ”mkataba waliosaini ni namna tutakavyofanya kazi kati ya JMAT na HWPL hii ni faida kubwa sana Jumuiya ya maridhiano na amani Tanzania itafanya kazi kimataifa na kuwa sehemu ya kusaidia amani ya dunia” amesema

Naye Mratibu wa taifa ambaye pia ni balozi wa amani duniani Fatama Kikkedes amesema ziara hiyo ameona ubaya wa vita kwani mwanamke ndiye anayekuwa mhanga mkubwa vita kwani anaumia mume watoto makazi na maisha yake hivyo amani iliyopo ni tunu kwani amani ikitoweka mwanamke ndiye anaathirika sana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!