Na Shomari Binda-Musoma
TIMU ya Rock City veteran kutoka mkoani Mwanza imetamba kutetea ubingwa wake wa bonanza la kumbukizi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Rock City ilichukua ubingwa mwaka jana katika bonanza la kumbukizi ya miaka 23 tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na kuzipiku timu nyingine 7 za kanda ya ziwa.
Akizungumza kwa njia ya simu na Mzawa Blog mshambuliaji wa timu hiyo Peter Mumbara amesema kwa namna walivyojipanga wanakwenda kutetea ubingwa wao.
Amesema kama walivyochukua ubingwa huo kwenye uwanja wa Karume mwaka jana wanakwenda kufanya hivyo tena mwaka huu.
Mumbara amesema mwaka huu wameimalika zaidi kutokana na mazoezi waliyoyafanya na hawajaona timu ya kuwazuia.
“Tumejiandaa vizuri na bonanza la mwaka huu na tunakwenda Musoma kutetea ubingwa wetu tuliouchikua mwaka jana”
“Tunajua wrnzetu nao wamejipanga Ila sisi Rock City veteran tumejipanga zaidi na tunakwenda kuchukua ubingwa kwa mara ya pili” amesema Mumbara.
Mmoja wa mratibu wa bonanza hilo,Katunzi Kiza amesema maandalizi yanaendelea vizuri ili kuweza kufanyika kwa bonanza hilo.
Amesema bonanza hilo litafanyoka kwa siku 2 oktoba 14 na 15 na kushirikisha timu 8 kutoka kanda ya ziwa na kuwaomba wadau kujitokeza kuweza kuchangia na kufanikisha