Home Kitaifa WANAWAKE MARA WATAJWA KUMVUSHA RAIS SAMIA ZIARA YA MBUNGE AGNESS MARWA ZANZIBAR

WANAWAKE MARA WATAJWA KUMVUSHA RAIS SAMIA ZIARA YA MBUNGE AGNESS MARWA ZANZIBAR

Na Shomari Binda

WANAWAKE mkoani Mara wametajwa kuwa ni “jeshi kubwa” linaloweza kumvusha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye uchaguzi wa 2025/2030

Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa “M-NEC” Mvita Mustapha wakati akizungumza na wajumbe wa UWT kutoka wilayani Rorya.

Wajumbe wa UWT wapo visiwsni Zanzibar ikiwa ni muendelezo wa ziara kwa viongozi wa UWT kutoka mkoani Mara inayoratibiwa na mbunge wa viti maalum Agness Marwa.

Amesema wanawake ni jeshi kubwa na ana Imani na wanawake wa mkoa wa Mara chini ya mbunge wa viti maalum Agnes Marwa kuwa 2025 watamvusha Rais Samia kwa asilimia 100.

Akiwa katika ofisi za CCM Tawi la Kizimkazi kushuhudia ziara iliyopewa jina la Mara To Zanzibar Royal Tour iliyoandaliwa na mbunge huyo amesema wanawake hao wameonyesha ujasili mkubwa.

Mustapha amesema amekutana na wanawake wa wilaya ya Rorya na kusalimiana nao na kuona namna ambavyo wapo tayari kumuunga mkono Rais Samia.

” Niwapongezeni sana wanawake kutoka wilayani Rorya kwa kufika hapa visiwani Zanzibar ili kujifunza mambo mbalimbali na kufanya utalii wa ndani.

“Nawaamini sana jeshi kutoka mkoani Mara na imani yangu ni kwamba mtakwenda kumvusha Rais Samia kwenye uchaguzi wa 2025”, amesema Mustapha.

Wakati huo huo mjumbe huyo wa NEC amempongeza mbunge Agness Marwa kwa ubunifu wa kuwapeleka wanawake Zanzibar kama kuunga juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazofanya na kuwataka wsnawake watakapo rudi mkoani Mara wafikishe salamu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!