Home Kitaifa WADAU WAUNGA SERIKALI MKONO KATIKA SEKTA YA ELIMU

WADAU WAUNGA SERIKALI MKONO KATIKA SEKTA YA ELIMU

Na Magrethy Katengu

Wadau wa elimu kuunga serikali katika suala la elimu kwa kuwasaidia wanafunzi kusoma nje ya nchi vyuo vikuu ikiwemo USA, UK Canada India lengo ni kuongeza wigo mpana wa kwa elimu

Akizungumza Jijini Dar es salaam Meneja Taasisi ya masuala ya Elimu ya S3 Education Fatema Salemwala katika maonesho ya vyuo Vikuu mbalimbali 30 vinavyokuja kila mwakakutoka nje ya Nchi kwa lengo la kutoa fursa kwa wanafunzi nchini kujiunga na Elimu ya juu nje ya nchi.

Fatema Salemwalla, amesema kuwa maonesho hayo yanalenga kuwasadia wanafunzi kupata uelewa mpana wa kozi ambazo wanahitaji kwenda kuzisoma nje ya nchi kwa kukutanisha moja kwa moja na wahusika wa vyuo hivyo bila malipo yeyote .

Bi Salemwalla amesema katika Maonesho hayo ya siku moja katika Hoteli ya Serena zaidi ya wanafunzi 500 kutoka shule mbalimbali wa kidato cha sita wametembelea na kuweza kukutana fursa mbalimbali za kielimu kutoka katika vyuo vikuu ikiwemo vya nchini Mauritius,UK,Canada na USA.India

“Maonesho tunayafanya mara mbili kwa mwaka,lengo ni kutoa fursa kwa vyuo hivi vikuu nje ya nchi kutangaza kozi zao,tunawaalika kwa wanafunzi kupitia shule zao kuja kutembelea maonesho haya,na sasa hivi teknolojia imekuwa kubwa,wanafunzi wanafanya utafiti mapema wa kujua kozi ambazo wanahitaji kusoma kabla hata hawajafika kwenye vyuo husika” amesisitiza

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliotembelea maonesho hayo akiwemo Maryam Suleiman anayesoma kidato cha sita katika shule ya Shaaban Robert Jijini Dar es salaam ambaye amesema kwamba maonesho hayo yamekuwa chachu kubwa na yatawasadia kama wanafunzi wa Tanzania kutimiza ndoto zao za kusoma nje ya nchi.

“Leo tumepata fursa kubwa ya kutambua vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi ambavyo vina kozi tunazozipenda na wazazi wetu wanao uwezo wa kuvilipia ambavyo vitatupa elimu ambayo itatupa mwanga wa kuja kuwekeza hapa nchini Tanzania” amesema Maryam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!