Home Kitaifa GST YATOA ELIMU YA MAJANGA YA ASILI MANYARA

GST YATOA ELIMU YA MAJANGA YA ASILI MANYARA

Maadhimisho ya Wiki ya Maafa Duniani 2023 kufanyika Manyara

GST yatoa wito kwa wananchi kupata elimu ya Majanga ya Asili

Katika kuadhimisha Wiki ya Maafa Duniani, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeanza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari za majanga ya Asiliya jiolojia hususan Matetemeko ya Ardhi ambayo hutokea katika maeneo mbalimbali nchini kwakuwa nchi yetu imepitiwa na Ukanda wa Bonde la Ufa la Afrika Mashariki.

Maonyesho hayo yameanza leo Oktoba 09, 2023 mjini Babati Mkoa wa Manyara na yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Oktoba 10, 2023 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.

Akizungumza katika maonesho hayo, Meneja wa Sehemu ya Mapping & Economic Geology na Mkuu wa Kitengo cha Majanga ya Asili ya jiolojia kutoka GST Bw. Gabriel Mbogoni amesema GST imeshiriki maonyesho hayo ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Majanga ya Asili ya Jiolojia kwa lengo la kupunguza athari zitokanazo na majanga hayo hususan katika kipindi hiki ambacho kumetolewa tahadhari ya uwezekano wa kutokea kwa mvua za Elnino.

Katika hatua nyingine Mbogoni ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda la GST ili kujifunza na kupata uelewa wa majanga ya Asili ya Jiolojia.

Maonesho hayo hufanyika Mwezi Oktoba Kila Mwaka ambapo kwa Mwaka huu yanafanyika Mjini Babati Mkoani Manyara ambapo yamebebwa na Kauli Mbiu isemayo “Imarisha Usawa kwa Uthabiti Endelevu” ambapo Kauli Mbiu hiyo inalenga kuhamasisha umuhimu wa kuwa na mikakati thabiti ya kupambana na umaskini na ukosefu
wa usawa ili kuweza kupunguza athari za maafa zitokanazo na matokeo ya umaskini,
ukosefu wa usawa na ubaguzi.

Maonesho hayo yanakwenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yaliyobebwa na Kauli Mbiu isemayo “Vijana na Ujuzi Rafiki wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu” pamoja na kilele cha mbio za Mwenge.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!