Home Kitaifa MATATIZO KWENYE NDOA NA MAHUSIANO MOJA YA VISABABISHI VYA MAGONJWA YA AFYA...

MATATIZO KWENYE NDOA NA MAHUSIANO MOJA YA VISABABISHI VYA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI

Na Shomari Binda-Musoma

MATATIZO na ugomvi kwenye ndoa na mahusiano yametajwa kama kisababishi cha magonjwa ya afya ya akili na wengine kupelekea kujitoa uhai.

Hayo yamesemwa na mganga wa manispaa ya Musoma Dk.Mustafa Waziri katika kuelekea siku ya magonjwa ya afya ya akili inayoanzimwa oktoba 10 kila mwaka.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Mzawa Blog ofisini kwake amesema visababishi vipo vingi lakini ugomvi kwenye ndoa na mhusiano ni moja ya visababishi.

Amesema kunapokuwa na ugomvi ndani ya ndoa na kwenye mahusiano wengine upelekea kupata msongo wa mawazo na kupata ugonjwa wa afya ya akili.

Mustafa amesema inapoyokea hali kama hiyo ni vyema kuwaona wataalam wa afya ya akili na wanasaikolojia ili kuweza kupata msaada.

Mganga huyo wa manispaa ya Musoma amesema kwenye hospital ya manispaa ya Musoma kipo kitengo ambacho Kinatoa msaada wa kisaikolojia kuwasaidia watu wenye changamoto ya afya ya akili.

Amesema licha ya matatizo kwrnye ndoa na mahisiano kuwa na wasiwasi,huzuni na magonjwa ya sonona upelekea kuwa na tatizo la afya ya akili.

“Tunashauri watu wasikae na matatizo bila kutafuta ushauri hii inaweza kupelekea kupata tatizo la afya ya akili na hata kupelekea wengine kujisitishia uhai”

“Hapa kwenye hospital yetu ya manispaa ya Musoma kipo kitengo ambacho kinasaidia matatizo haya pamoja na ustawi wa jamii ambapo msaada unatolewa” amesema Dkt.Mustafa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!