Home Kitaifa KILIMO CHA UMWAGILIAJI CHATAJWA KUWA SULUHISHO UPATIKANAJI WA CHAKULA

KILIMO CHA UMWAGILIAJI CHATAJWA KUWA SULUHISHO UPATIKANAJI WA CHAKULA

Na Shomari Binda-Musoma

KILIMO cha umwagiliaji kimetajwa kuwa suluhisho la upatikanaji wa chakula cha uhakika hapa nchini.

Licha ya uhakika huo wa chakula lakini kilimo hicho cha umwagiliaji kinatoa chakula cha kutosha na kufanikisha kupatikana kwa bei nafuu.

Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo kuhusiana na upatikanaji wa chakula.

Amesema tangu miaka ya nyuma Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alidhamiria kujenga miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kwenye bonde la Bugwema lililoko Musoma Vijijini ili kufanikisha kilimo hicho.

Muhongo amesema ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ilianza kujengwa mwaka 1974 lakini baadae mradi huo ukasimama.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, ameiomba serikali ifufue mradi huo ambapo imekubali na kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha (2023/2024) kazi za feasibility studies na designing zimeanza.

Amesema jimbo la Musoma vijijini lina mabombe makubwa mawili yenye vigezo vyote vya uanzishwaji wa kilimo kikubwa cha umwagiliaji ya Bugwema na Suguti.

“Tunaishukuru serikali yetu kwa kuamua kutenga bajeti kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji ambalo ndio suluhisho la upatikanaji wa chakula cha uhakika”

“Tutaendelea kufanya ufatiliaji ili mabonde yetu ya Bugwema na Suguti tuweze kufanya kilimo cha umwagiliaji na kufikia malengo” ,amesema Muhongo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!