WATALII Na wawekezaji sekta ya Utalii waaswa kuwekeza katika utalii wa Kanda za nyanda za kusini ili kuweza kutangaza vivutio vilivyopo mikoa ya kusini na kuendelea kuongeza idadi kubwa ya watalii nchini.
Akizungumza na Mzawa blog katika siku ya pili ya Maonesho ya Saba ya Swahili International Tourism Expo – S!TE, 2023 Oktoba 7,2023 Katika Ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es Salaam, Afisa kutoka Bodi ya Utalii Sane Tobico amesema bado inahitaji nguvu kubwa ya kuhamasisha watalii kutembea vivutio vilivyopo kusini na kupitia mradi wa usimamizi wa Utalii kusini ( REGROW) umeonesha wazi kuwa wataendelea kukuza na kujenga uwelewa kwa watalii kutembelea hifadhi hizo za kusini mwa Tanzania na kuwekeza.
“Mradi wa kuboresha na usimamizi Maliasili na kukuza utalii kusini mwa Tanzania (REGROW) kwa kushirikiana na wadau wa Utalii unaendelea kukuza utalii na kuyapa kipaumbele maeneo ya kusini ili kuwawezesha watalii na wawekezaji kutembelea vivutio hivyo.”
Hata hivyo amesema Mradi huo wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na kukuza utalii kusini mwa Tanzania (REGROW) kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kw kushirikisha Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,Wakala wa huduma za misitu(TFS) , Taasisi ya utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) ,Bodi ya Utalii nchini(TTB), Tume ya Umwagiliaji (NIRC pamoja na bodi ya Maji ya bonde la Rufiji (RBWB).
Kwa upande wake Msimamizi shughuli za hifadhi ya Utalii Hifadhi ya Nyerere Titindaga George amewaomba wadau wa utalii kutembelea banda hilo ili kupata elimu mbalimbali kuhusiana na uwekezaji na kutembelea vivutio hivyo vya kanda ya kusini mwa Tanzania.
“Kanda ya kusini kuna vivutio mbalimbali vinavyopatikana ikiwemo Hifadhi ya katavi,udzungwa,Mikumi,kitulo na Ruaha hivyo watali wafike kuona vivutio hivyo ili viweze kujitangaza zaidi na taifa lifaidike kupitia utalii wa nyanda za kusini mwa Tanzania .”
Pia amebainisha kuwa kuna fursa nyingi kupitia Banda hili kwa ambae anafika ataunganishwa Moja Kwa moja na wadau wa utakuwa ili kuwekeza katika Utalii .
Nae Mkurugenzi kutoka Kampuni ya Utalii Mkoa wa Njombe (RAMIKA) amesema Maonesho haya yanatoa fursa mbalimbali ya kuwakutanisha wadau wa Utalii kubadilishana uzoefu na Kuongeza Elimu ya namna ya kuwahudumia watalii wanaofika katika vivutio vya Utalii nchini.
Aidha ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kuona ipo tija ya kufanyika kwa Maonesho haya kwa mara ya Saba lengo ni kutoa semina kwa wahudumu hao wa Utalii na kuboresha sehemu mbalimbali lengo hasa kubwa kutoa kipaumbele na kujitangaza kwa vivutio hivyo kwa ukubwa zaidi ili kuwapa nafasi wadau kuwekeza.