Home Michezo RC MTANDA AWAPA NENO MAKOCHA BIASHARA UNITED WAKIIFUNGA STEND UNITED 1-0

RC MTANDA AWAPA NENO MAKOCHA BIASHARA UNITED WAKIIFUNGA STEND UNITED 1-0

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara Said Muhamed Mtanda amelishauri benchi la ufundi la Biashara United kuongeza kasi ya kunoa safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi ya Championship dhidi ya Stend United na kushinda bao 1-0 amesema bado washambuliaji wanahitaji kunolewa zaidi.

Amesema licha a kushinda dhidi ya Stend kuna nafasi ambazo hazikutumiws vizuri za kupata mabao zaidi.

Mtanda amesema ligi hiyo ni ngumu na ni vizuri kuchukua pointi na mabao mengi ya kutosha mapema na sio kusubili mwisho wa msimu.

Amesema.washambuliaji wanapaswa kutumia nafasi wanazopata vizuri ili kupata ushindi wa mabao mengi hivyo benchi la ufundi linapaswa kuwaongezea nguvu.

“Ushindi tumepata lakini bado ni mwembamba tuwaongezee mbinu washambuliaji wetu ili kila nafasi tunayoipata uwanjani tuweze kuifanyia kazi”

“Tunahitaji kurudi ligi kuu msimu ujao ili tuendelee kupata burudani kwenye uwanja huu na mkoa utaendelea kutoa ushirikiano ili kufikia malengo”, amesema Mtanda.

Kocha wa makipa wa timu hiyo Ivo Mapunda amesema benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Amani Josia watakwenda kufanyia kazi ushauri wa mkuu wa mkoa.

Amesema timu inaendelea kuimalika na kuwa na matumaini ya kufanya vizuri lakini kama benchi la ufundi wanapokea ushauri wa kuimalisha kikosi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!